Wapogolo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Wapogolo ni kabila la watu kutoka kusini-kati ya nchi ya Tanzania, hususan mkoa wa Morogoro.

Lugha yao ni Kipogolo.

Mwaka 1987 idadi ya Wapogolo ilikadiriwa kuwa 185,000

Historia[hariri | hariri chanzo]

Inasemekana asili yao ni Afrika Magharibi, hasa katika nchi ya Senegal, pia Afrika ya Kati (Kongo). Kuna mila nyingi Senegal na ngoma zake nyingi zinafanana na Sangula.

Sababu ya kuhamia Tanzania ilikuwa utafutaji wa ardhi ya kilimo na mabadiliko ya hali ya hewa. Waliendelea kuhama zaidi na wengine walikimbilia pia Zambia, Zimbabwe na Malawi. Ndiyo maana kuna ukoo mkubwa wa Matimba kule Malawi na Zimbabwe.

Utamaduni[hariri | hariri chanzo]

Chakula kikuu cha Wapogolo ni wali na samaki na makazi yao ni sehemu za ardhi zenye rutuba ambazo hufaa kwa kilimo cha mpunga na shughuli za uvuvi.

Wapogolo wakati wa masika huwa na shughuli za utafutaji, hasa shughuli za kilimo na kwa asili ni watu wanaolima kwa ujamaa, yaani kaya moja huweza kupika togwa na kualika kaya nyingine ziweze kusaidia shughuli za kilimo kwa togwa. Wakati wa masika kaya zote huwa na kazi za uzalishaji kwa shughuli za kilimo kwa kulima mpunga na wakati wa kiangazi sherehe nyingi huwa zinafanyika katika jamii za Wapogolo.

wakati wa sherehe za kabila la Wapogolo ngoma aina ya sangula hupigwa na hii ndiyo ngoma ya asili ya kabila wa Wapogolo. Ngoma hiyo ya sangula hupigwa wakati wa furaha kama vile kwenye shughuli za sherehe za mavuno, sherehe za kusimikwa kiongozi wa ukoo, matambiko na n.k.

Katika kaya za Kipogolo wakati wa jioni wazee hupenda kukaa na wajukuu kwa lengo la kuwasimulia mambo ya kale yenye mafunzo ili kuwajenga watoto hao wanapokuwa wakubwa kujua nini wanapaswa kufanya. Wakati wa mazungumzo hayo huwa wanatafuta pepeta. Pepeta ni kitafunwa kinachotokana na zao la mpunga, huandaliwa kwa kuchukua mpunga mteke (mpunga usiokomaa) na kuukaanga, kisha kuutwanga na kutengeneza pepeta. Ni moja kati ya kitafunwa cha kiburudisho kwa kabila la Wapogolo.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wapogolo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.