Waluguru

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Waluguru ni kabila la Tanzania wanaoishi katika mikoa ya Morogoro na Pwani, hasa kwenye Milima ya Uluguru (Wilaya ya Mvomero) na katika wilaya ya Morogoro vijijini ukianzia Matombo kuelekea Dutumi hadi Bwakila Juu. Kuna makundi makubwa mawili ya Waluguru. Makundi hayo ni Waluguru wanaoishi milimani na wale wanaoishi mabondeni. Waluguru wa milimani wanapatikana katika maeneo ya Mgeta, Kolero,baadhi ya maeneo ya Matombo na Kiroka, na pembezoni mwa Milima ya Uluguru hasa ile ya Tao la Mashakiri. Katika mfumo wa kifamilia Waluguru hufuata ukoo kwa mama yaani kwa kiingereza ''matrilineare''. Hatahivyo, mtoto wa kiluguru huitwa jina la ukoo wa baba yake. Yaani: Waluguru wana 'mtala' na ukoo. Mtala ni jina la ukoo wa baba ambalo ndilo analoitwa mtoto. Kwa mfano: mtoto akiitwa 'Kobero' jina hili ni mtala na si la ukoo wake kwani 'kobero' ni jina analopewa mtoto ambaye baba yake ni 'mmadze'. Halikadhalika, mtoto akiitwa 'Mkude' jina hili ni mtala wa ukoo wa 'Wamwenda' lakini si la ukoo wa mtoto. Hivyo basi, kwa Waluguru baba hutao jina na mama hutoa ukoo: jina ni la ukoo wa baba, na ukoo ni wa mama!

Waluguru wanapenda kuishi pamoja na kushirikiana. Pia hupensda kunywa pombe na kushiriki kwenye sherehe za kimila.

Tamaduni na mila zao hufahamika sana katika suala la kucheza ngoma za asili kati ya Oktoba hadi Januari, hasa wale wanaoishi katika vijiji vya Longwe, Tegekelo, Mgeta, Kumba, Singisa, Bwakira, Kolero, Nyamighadu na vinginevyo vingi.

Vyakula vya asili ni magimbi, matuwi na mahimbi pamoja na mihogo.

Lugha yao ni Kiluguru.

Upande wa dini, kwa kawaida wale wa wanaoishi mabondeni ni Waislamu na wale wa milimani ni Wakristo, hasa wa Kanisa Katoliki.