Mpishi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mpishi akipika chakula.

Mpishi ni mtaalamu au ni mtumishi ambaye anahusika na maandalizi ya vyakula mbalimbali. Neno linaloweza kumtaja mkuu wa wafanyakazi hao ni mpishi mkuu.

Pengine kazi hiyo inatazamwa kuwa ya chini sana kama kazi ya kimwili zaidi. Zamani kazi ya upishi ilikuwa inahusisha wanawake ila kwa sasa ni kazi ya wote, wawe wa kike au wa kiume, tena wapishi bora duniani ni wanaume.

Mpishi ana wajibu wa maandalizi ya chakula cha kila siku, pamoja na matukio mengine maalum, kama sherehe za harusi, kipaimara, mahafali n.k. Pia mpishi anawajibika kuwa na utaratibu wa kusambaza chakula maeneo mbalimbali.

Mpishi ananatakiwa awe mbunifu wa vyakula mbalimbali ili kupikia wateja hata kama si utamaduni wao.

Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mpishi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.