Nenda kwa yaliyomo

Wamwera

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Wamwera ni kabila la watu wa Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Lindi, hasa kwenye Wilaya ya Nachingwea, Lindi Vijijini na Ruangwa.

Wamwera huwasiliana kwa lugha yao ya Kimwera (wao wanasema Shimwera), lugha ambayo ina muundo unaoeleweka upande wa sarufi na matamshi yake, tena kwa urahisi sana.

Wanajitahidi kudumisha mila na desturi zao. Wamwera ni maarufu kwa kufuata mfumo jike, ambao mwanamke ndiye mwenye nguvu na anapewa umiliki wa watoto na ndiye mtawala mkuu, hivyo watoto hutumia majina ya koo za mama zao.

Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wamwera kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.