Wazanaki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mwalimu Nyerere wa kabila la Kizanaki alopingana na dhana ubaguzi wa kikabila nchini Tanzania

Wazanaki ni kabila la watu kutoka eneo la kaskazini-magharibi mwa nchi ya Tanzania, jamii ya Wakurya.

Mwaka 1987 idadi ya Wazanaki ilikadiriwa kuwa 62,000 [1]. Lugha yao ni Kizanaki.

Hili ni kabila la Mwl. Julius Kambarage Nyerere aliyezaliwa mwaka 1922 na alipata elimu ya kikoloni. Mkoa aliozaliwa Nyerere ni Mara, kata ya Butiama.

Mwaka [1961] aliipatia Tanganyika uhuru, halafu mwaka 1964 Tanganyika na Zanzibar ziliungana kuunda Tanzania. Mwl. Julius Kambarage Nyerere alifariki mwaka 1999 na kifo chake kilihuzunisha watu wa taifa lote la Tanzania.

Vifaa alivyotumia katika kazi tofauti za utawala wake vilikuwa sehemu ya ukumbusho wa baba wa taifa la Tanzania. Vifaa hivyo ni kama vile fimbo aliyokuwa akitembea nayo kila aendapo. Kitu cha pili ni kiti alichopenda kukalia wakati wa kupumzika. Vitu hivyo vipo katika eneo aliloishi na vinawavutia watalii kwa kiasi kikubwa na kuongeza uchumi wa nchi.

Kaburi lake lipo karibu na nyumbani kwake na makaburi ya ndugu zake yapo nyumbani kwake pia.

Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wazanaki kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.