Wamatumbi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Mkoa wa Lindi Manispaa

Wamatumbi ni kabila la watu wa Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Lindi. Lugha yao ni Kimatumbi.

Wengi wao wanapatikana wilaya ya Kilwa (Kilwa Masoko) katika vijiji vya Kipatimu, Namayuni, Chumo na Nandete.

Wamatumbi huishi kwa kutegemea kilimo. Ni wakarimu sana na wanaishi kwa kusaidiana na kutegemeana.

Miongoni mwao wapo Wakristo na Waislamu na dini hizi zimeenea kulingana na maeneo ambayo watawala wa zamani yaani wakoloni wamepita.

Flag of Tanzania.svg Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wamatumbi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.