Wilaya ya Kilwa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kwa matumizi mengine ya jina hili tazama Kilwa

Mahali pa Kilwa (kijani) katika mkoa wa Lindi.
Ramani ya Kilwa

Wilaya ya Kilwa iko katika Mkoa wa Lindi, takriban kilometa 220 kusini mwa Dar es Salaam. Kilwa imepakana na Mkoa wa Pwani upande wa kaskazini, Bahari ya Hindi upande wa mashariki, wilaya ya Lindi Vijijini upande wa kusini na wilaya ya Liwale upande wa magharibi. Wakati wa sensa ya nwaka 2012, wilaya hii ilikuwa na wakazi 190,744[1] (mwaka 2002 waliohesbiwa 171,850 ).

Makao makuu ya wilaya ni Kilwa Masoko.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Wilaya hii ina sehemu za kihistoria ambazo ni hasa

  • Kilwa Kisiwani - ambayo ni mfano bora wa miji ya Waswahili wa kale uliojulikana kimataifa tangu karne ya 13 BK
  • Kilwa Kivinje - iliyokuwa makao makuu ya eneo chini ya masultani wa Zanzibar na wakati wa ukoloni
  • Songo Mnara - maghofu ya mji wa Waswahili wa kale

Uchumi[hariri | hariri chanzo]

Wakazi wengi hutegemea kilimo na uvuwi. Mazao yanayolimwa hasa ni pamoja na muhogo, mahindi, mtama na mpunga. Hata hivyo uzalishaji wa chakula hautoshelezi mahitaji ya wakazi. Sababu za upungufu ni kuongezeka kwa watu pamoja mitindo ya kilimo cha kimila ambako mashamba ni madogo, kwa wastani ekari 2, yakilimwa kwa mkono tu. Sehemu kubwa za wilaya kuna ardhi isiyo na rutba kubwa ambayo haushiki maji vizuri. Penye udongo mweusi mzuri karibu na Makangaga, Liwiti, Matandu, na Mbwemkuru inawezekana kulima mpunga. Kuna maeneo katika Milima ya Matumbi ambako miti ya matunda kutunzwa, hasa minazi na michungwa. Karibu na Likawage, Nanjirinji, Nainokwe, Njinjo na Singino Hill watu wanavuna pia korosho. Upatikanaji wa inzi za tsetse ni kizuizi kwa ufugaji.[2]

Kuna pia majaribio ya kupana vchaka vya Jatropha curcas kama zao la nishati[3].

Gesi asilia huzalishwa kwenye Kisiwa cha Songosongo. Gesi hii inapelekwa hasa Dar es Salaam kwa uzalishaji wa umeme; lakini kuna pia kituo cha umeme kinachoendedhwa na gesi ya Songosongo kilichopo kwenye kata ya Somanga kikihudumia wilaya hii.

Utawala[hariri | hariri chanzo]

Wilaya hii ina kata zifuatazo (idadi ya wakazi 2012 katika mabano):

Kata za Namayuni na Somanga zilianzishwa baada ya sensa ya 2012 kwa hiyo hakuna namba za kulingana.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Sensa ya Tanzania ya 2012. Jalada kutoka ya awali juu ya 2010-02-10. Iliwekwa mnamo 2010-10-30.
  2. Kilwa District, kifungu Agriculture Archived 26 Aprili 2019 at the Wayback Machine., tovuti ya mpingoconservation.org
  3. Jatropha plantations in Kilwa district. Jalada kutoka ya awali juu ya 2019-04-26. Iliwekwa mnamo 2019-04-26.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Kata za Wilaya ya Kilwa - Mkoa wa Lindi - Tanzania

Chumo | Kandawale | Kibata | Kikole | Kinjumbi | Kipatimu | Kiranjeranje | Kivinje | Lihimalyao | Likawage | Mandawa | Masoko | Miguruwe | Mingumbi | Miteja | Mitole | Namayuni | Nanjirinji | Njinjo | Pande | Somanga | Songosongo | Tingi


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Lindi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Wilaya ya Kilwa kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.