Wakw'adza
Mandhari
Wakw'adza (huitwa pia Waqwadza, Wangomvia) walikuwa kabila dogo la watu wa Tanzania ambao waliishi kwanza katika Mkoa wa Manyara, Wilaya ya Mbulu, halafu katika Mkoa wa Dodoma, Wilaya ya Bahi.
Lugha yao ilikuwa Kikw'adza, moja kati ya lugha za Kikushi, iliyokufa kati ya miaka 1976 na 1999, kwa sababu katika karne ya 20 Wakw'adza walijichanganya na majirani wao Wagogo na Wasandawe[1]. Haieleweki kama bado kuna watu wanaojiona kuwa wa kabila hilo. Ndugu zao wa jirani ni Wairaq.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]| Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Wakw'adza kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |