Wahehe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Wahehe mnamo 1906.

Wahehe ni watu wa kabila la Tanzania ambalo kiasili linaishi katika wilaya za Mkoa wa Iringa, yaani Iringa mjini, Iringa vijijini, Kilolo na Mafinga.

Ni moja kati ya makabila yaliyotokea kwenye bonde la mto Rufiji. Ndiyo sababu wanazika wafu wao wakielekea mashariki.

Lugha yao (Kihehe) imegawanyika kiasi fulani katika lahaja (matamshi) tofautitofauti kutokana na maeneo ambayo huzungumzwa. Inafanana kimatamshi na kimaana hasa na lugha ya Kibena iliyopo mkoani Njombe, lakini pia na lugha ya Kisangu iliyopo mkoani Mbeya.

Pamoja na Wabena wanahesabika kuwa zaidi ya watu milioni moja.

Wengi wao ni wafuasi wa Ukristo, hasa wa Kanisa Katoliki (Jimbo Katoliki la Iringa).

Katika historia Wahehe ni maarufu kwa jinsi walivyopambana na Wajerumani walioteka maeneo yao, k.m. katika pigano la Lugalo mwaka 1891. Kiongozi wao alikuwa Chifu Mkwawa.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Flag of Tanzania.svg Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wahehe kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.