Wajita

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Wajita ni kabila la watu wa Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Mara. Lugha yao ni Kijita.

Wajita wana muingiliano mkubwa na makabila kama Waha, Wahaya, Wanyankole, Wanyoro, Watoro, Wakerewe, Wahangaza, Wanyambo, Wazinza, Wakara, Wakabwa, Waruri, Wasweta, Wasimbiti, Wakwaya na kadhalika. Kulingana na historia yao wengi waweza kuitana wajomba. Bila kusahau Wajaluo ambao ni watani wao.

Wajita nao wana koo nyingi sana kama Bhajigabha, Bhegamba, Bhatata, Bhagaya, Bharamba, Bhaanga, Bhalinga, Bhaila, Bhalaga, Bhatimba na wengineo.

Wajita ni watu wachapakazi sana na wasiopenda dhihaka kwenye kazi, wenye msimamo sana na wapole, ila wakali sana wanapoonewa, wenye kupenda utani.

Historia ya Wajita[hariri | hariri chanzo]

Inasemekana makabila mengi ya mkoani Mara si Wabantu asilia lakini walipokuja mkoani Mara wengine walichagua kuzungumza lugha ya kijita na lugha nyingine za Mara.

Inawezekana badhi ya Wajita wana asili toka Rwanda, Burundi, Uganda, Sudan kaskazini kama Wanubi na pia Niger kama Wahausa na Nigeria kama Waigbo.

Kati ya vijiji vingi vya Wajita utavikuta pia Rwanda, Uganda, Burundi. Kati ya vijiji hivyo mfano ni Rusori, Buringa na vinginevyo vingi tu.

Wajita wengi nao wana koo zao ambao hata wakienda Rwanda, Uganda, Niger, Burundi ni rahisi kutambua koo zao kulingana na miiko yao. Kama jamii zingine zozote zilizoweza tambua ndugu zao kutokana na miiko, mfano ya nyama ama vyakula vingine. Mfano: Wajita wa koo za Rusori wengi kuna samaki hawali, ila kulingana na mazingira ya siku hizi watu kutoelewa wanajikuta wakila samaki. Mila hizo pia ziko kwa Wanyoro wengi, Watoro na Wanyambo. Wajita wengine hawawezi kuua chatu na ni mwiko kabisa kama vile kwa Wahausa, Waigbo, na pia wengine wanaheshimu sana chura kama ilivyo kwa koo nyingine nchini Rwanda.

Wajita wenye asili ya Kibantu ni wengi sana na wanatokea katika koo za Bahitira. Mfano Waruri wengi ni Wabantu na wanatokea Bururi na ni kabila ambalo pia liko Uganda.

Pia wapo ambao wana asili ya Kush. Mfano: inaaminika Wajita wa kwanza kufika Musoma na wanaojiita Original ni wale wenye asili ya Warusori; mpaka sasa wao ni weupe na warefu sana, wapo na pua zao za kuchongoka. Yasemekana hao si Wabantu, wana asili ya Kinubi na Ethiopia na wengine pia wanatokea Bunyoro na wengine wakaenda Rwanda na Burundi.

Wajita wengi wenye asili ya Banyoro ni warefu sana, ingawa wengine ni weusi siku hizi kutokana na mchanganiko. Wenye asili ya Nubia na hao Banyoro zamani walikuwa kama Waarabu kwa mbali, ambao wengi wasemekana ni hao Warusori.

Watu ambao wametokea Ethiopia, wana asili ya Kushi na wana mwingiliano wa karibu na Watsi, ni Watimba, Watimbaru kutoka Ukurya. Watimba ndio ukoo mkubwa katika kabila la Wajita, ambao asili yao walitokea Hemit, Ethiopia.

Wajita pia walikuwa na utawala wao, ambapo watemi wao walikuwa wa ukoo wa Bhatimba, ambao ni Kusaga, Makunja, Magai, Majinge na wengineo. Uchifu wao uko Majita kijiji cha Bwasi.

Watu maarufu kutoka kabila la Wajita[hariri | hariri chanzo]

 1. Chinuno Magoti, daktari wa binadamu
 2. Mkama, aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa CCM
 3. Bitta John Musiba, aliwahi kuwa mchezaji wa Simba Sports Club na Taifa Stars
 4. Isaac Muyenjwa Gamba, Mtangazaji wa DW, Bonn, Ujerumani
 5. Kangi Alphaxard Lugola, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
 6. Munasa Sabi Munasa, Kada wa CCM
 7. Sospeter Gomborojo Massambu, mwanasiasa
 8. Aristablus Musiba, mwandishi wa riwaya
 9. Charles Majinge Kusaga, mkurugenzi wa hospitali ya Bugando, mwenyekiti wa bodi ya wadhamini hospitali ya Mhimbili .
 10. Joseph Kusaga, mkurugenzi na mmliki wa Clouds Media
 11. Donald Mapigano, jaji mkuu mstaafu wa mahakama kuu Tanzania.
 12. Riziki S. Majinge, mwandishi wa vitabu vya sheria Ulaya, pia mwanaharakati
Flag of Tanzania.svg Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wajita kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.