Nenda kwa yaliyomo

Simba S.C.

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nembo ya timu ya soka ya Simba SC

Simba Sports Club ni timu ya soka iliyo na makao makuu katika mtaa wa Msimbazi, Kariakoo, katika jiji la Dar es Salaam nchini Tanzania inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara ambapo ilianzishwa mwaka 1936, ikiitwa kwanza Eagles na baadaye tena iliitwa Dar Sunderland. Mwaka 1971 ikaibadilisha jina lake kabisa na kuitwa, Simba Sport Club (ambalo linamaanisha Lion kwa Kiinɡereza).

Simba Sports Club ni mojawapo ya timu kubwa ya mpira wa miguu nchini Tanzania, wapinzani wao wanaitwa Younɡ Africans.

Ni mabingwa wa taifa mara 18 tena ni mabingwa mara 6 katika kombe la Kagame.[1]

Mechi zao za nyumbani zinachezwa kwenye viwanja viwili, Uwanja wa Uhuru na Uwanja wa Taifa.

Mabadiliko ya utawala

Klabu ya soka ya Simba imesajiliwa kwa mujibu wa sheria namba 12 ya baraza la michezo la taifa ya mwaka 1967 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 1971. Katiba ya sasa ya timu ya Simba iliandikwa mwaka 2018 na kupitishwa tarehe 20 mayi 2018 na msajili wa vyama vya soka na klabu, na kisha kusajililiwa na wakala wa usajili, ufilisi na udhamini (RITA). Safari ya timu ya soka ya Simba kuelekea mabadiliko ilianza mwaka 2016 ambapo Kamati kuu kwa wakati ule ilibaini kwamba klabu iliendeshwa nje ya misingi na dira yake, hivyo kupelekea kushindwa kutimiza matarajio ya wadau wake, jambo lililopelekea kuwepo na ulazima wa kufanya mabadiliko ya kisasa kwa ajili ya maendeleo ya klabu.

Kamati kuu iliteua wajumbe wa kujitolea na wataalamu kwa ajili ya kufanya utafiti ili kubaini chanzo cha kutetereka kwa klabu ikiwemo kuzorota kwa uongozi, maendeleo hasi ya kiufundi, hali mbaya ya kifedha na kisha kupendekeza namna ya kufanya mabadiliko ili kuinusuru klabu. Kutokana na ripoti kamili na mapendekezo yaliyotolewa na Kamati ya mabadiliko mnamo Septemba 2016; Klabu ya soka ya Simba ipo katika mchakato wa mabadiliko hayo kwa kubadili mfumo wake wa kisheria na kiuendeshaji kutoka mfumo wa wanachama na kuwa kampuni ya dhima ya umma inayojulikana kama Simba Sports Club Limited, ambayo imeundwa na pande mbili; wanachama wakimiliki asilimia 51 ya hisa ambapo kati ya hizo, asilimia 10 zimelipiwa zote na kubaki asilimia 41, huku mwekezaji akimiliki asilimia 49. Mabadiliko yote yalifanyika kupitia mchakato wa wazi wa kutangaza zabuni na kusimamiwa na kamati maalumu ya uwekezaji wa klabu.

Kabla ya kupokea zabuni, kamati maalumu ya uwekezaji ya timu ya soka ya Simba, iliteua kamati ya kufanya tathmini ambayo ilijumuisha wajumbe watano wakiwa na jukumu la kufanya tathmini na kuleta mapendekezo kwenye kamati ya uwekezaji kwa kubainisha zabuni gani ilikuwa na faida kiuchumi. Zabuni iliyopata tathmini ya juu zaidi ilikuwa ni ya ndugu Mohammed Dewji ambayo ilikubalika kwa kukidhi vigezo vya tathimini kama vilivyobainishwa kwenye nyaraka za zabuni.

Mchakato wa kufanya tathmini ulipitia hatua zifuatazo: Tathmini ya hisa, mkakati wa kiufundi, mpango wa kifedha na mwisho ilikuwa hatua ya makubaliano. Tarehe 2 Novemba 2018, Simba Sports Company Limited ilijumuishwa na kuwa na wanahisa wawili wakijulikana kama Simba Sports Club Holding company limited ikimiliki asimilia 10 ya hisa zilizolipiwa na asilimia 41 ambazo hazijalipiwa jumla hisa 51, na Mo Simba Company Limited ikimiliki asilimia 49 ya hisa zikiwa zote zimelipiwa. Mchakato wa mabadiliko haya upo katika hatua za mwisho kukamilika.

Kama sheria inavyoelekeza katika kifungu cha 11 cha sheria ya ushindani wa biashara ya mwaka 2003; klabu ya soka ya simba: Imeomba idhini kutoka tume ya ushindani wa biashara kuhakikisha kwamba mchakato wa mabadiliko hauangukii katika ujumuishaji wa hisa (merger and acquisition) Inazingatia kanuni za mamlaka ya mapato nchini Tanzania (TRA) kuhusu uhamishaji wa mali Imeanza zoezi la uhakiki ili kutambua wanachama hai wa klabu ambao watanufaika na hisa. Mchakato huu unaendelea vizuri na wanachama pamoja na mashabiki wa timu ya Simba wameanza kushuhudia mabadiliko chanya ndani ya klabu yao pendwa. labu

Utawala

Simba Sports Club imebadilisha utawala au usimamizi wake kutoka kutawaliwa na mashabiki na badala yake kusimamiwa na mwanahisa aitwae Mohammed Gulam Dewji.

Katika muundo huu wa utawala wa Simba Sports Club imeuza hisa zake 49% kwa Mohammed Gulam Dewji huku wanachama wa Simba wakibakiwa na 51%.

Wachezaji

Note: Flags indicate national team as has been defined under FIFA eligibility rules. Players may hold more than one non-FIFA nationality.

Na. Nafasi Mchezaji
36 Moroko GK Ayoub Lakred
31 Tanzania GK Ahmed Feruzi
1 Tanzania GK Ally Salim
30 Tanzania GK Hussein Abel Thomas
28 Tanzania GK Aishi Manula
12 Tanzania DF Shomari Kapombe
5 Tanzania DF Israel Patrick
3 Tanzania DF David Kameta
15 Tanzania DF Mohamed Hussein
29 Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DF Henock Inonga Baka
6 Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo MF Patrice Ngoma
16 Tanzania DF Hussein Kazi
26 Tanzania DF Kenedy Juma
4 Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo MF Jean Baleke
20 Kamerun DF Che Malone
19 Tanzania MF Mzamiru Yassin
38 Tanzania FW Kibu Denis
13 Tanzania MF Abdallah Hamisi
8 Mali MF Sadio Kanoute
24 Côte d'Ivoire MF Kouame Kramo
11 Msumbiji MF Luis Miquissone
17 Zambia MF Clatous Chama
10 Burundi FW Saido Ntibazonkiza
14 Tanzania FW Mohamed Mussa
22 Tanzania FW John Raphael Bocco
7 Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo FW Leandre Willy Essomba Onana

Marejeo

  1. Tanzania - RSSSF

Viungo vya nje

Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Simba S.C. kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.