Kariakoo
Kata ya Kariakoo | |
Mahali pa Kariakoo katika Tanzania |
|
Majiranukta: 6°49′26″S 39°14′56″E / 6.82389°S 39.24889°E | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Mkoa | Dar es Salaam |
Wilaya | Ilala |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 10,246 |
Kariakoo ni kata ya wilaya ya Ilala katika Mkoa wa Dar es Salaam, Tanzania, yenye postikodi namba 11106.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 10,246 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 13,780 waishio humo.[2]
Kariakoo inajulikana kutokana na soko kubwa.
Asili ya jina
[hariri | hariri chanzo]Jina la eneo hili ni la kihistoria: linatokana na neno la Kiingereza "carrier corps", yaani kikosi cha wapagazi waliobeba mizigo ya jeshi wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia.
Pande zote vitani walitumia malakhi ya wapagazi waliokodishwa au kulazimishwa kufanya huduma hii.
Baada ya vita wapagazi kadhaa walipewa maeneo ya kujenga nyumba kwenye miji mbalimbali na hivyo majina kama "Kariakoo" au "Kariokor" (Nairobi) yanapatikana katika miji mbalimbali ya Afrika ya Mashariki.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://www.nbs.go.tz/
- ↑ http://www.meac.go.tz/sites/default/files/Statistics/Tanzania%20Population%20Census%202012.pdf Ilihifadhiwa 2 Januari 2004 kwenye Wayback Machine. Wilaya ya Ilala - Mkoa wa Dar es Salaam
Kata za Wilaya ya Ilala - Tanzania | ||
---|---|---|
Bonyokwa | Buguruni | Buyuni | Chanika | Gerezani | Gongolamboto | Ilala | Jangwani | Kariakoo | Kimanga | Kinyerezi | Kipawa | Kipunguni | Kisukuru | Kisutu | Kitunda | Kivukoni | Kivule | Kiwalani | Liwiti | Majohe | Mchafukoge | Mchikichini | Minazi Mirefu | Mnyamani | Msongola | Mzinga | Pugu | Pugu Station | Segerea | Tabata | Ukonga | Upanga Magharibi | Upanga Mashariki | Vingunguti | Zingiziwa |
Makala hii kuhusu maeneo ya Dar es Salaam bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Kariakoo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno. |