Laki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Lakhi)
Rukia: urambazaji, tafuta

Laki (pia Lakhi) ni neno lenye asili ya Kihindi linalotumika kutaja namba 100,000, ambayo inafuata 99,999 na kufuatwa na 100,001. Inaweza kuandikwa pia 105.

Kwa mfano, Mji una wakazi laki tano, yaani mia tano elfu.

Namba 650,000 inaweza kusomwa "laki sita na nusu".

Neno limeingia katika Kiswahili kutokana na historia ndefu ya mawasiliano ya kibiashara kati ya Bara Hindi na pwani ya Afrika ya Mashariki.

Pengine inasikika kwamba wingi wake ni neno lukuki, lakini matumizi ya kawaida ni tofauti.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]