Tabata

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Tabata ni kitongoji cha jiji la Dar es Salaam, Tanzania. Kitongoji hicho kipo katika wilaya ya Ilala, kata ya Segerea katika Tarafa ya Ukonga.

Kitongoji cha Tabata kimegawanyika katika maeneo mengi; baadhi ya hayo ni kama Tabata Bima, Tabata Kimanga, Tabata Shule, Tabata Segerea na mengineyo.

Tabata Kimanga ni eneo ambalo lina watu wengi, wakiwemo wafanyabiashara, na shule za serikali zipatazo nne ambazo ni: Kimanga, Tumaini, Kisukuru na Makoka.

Pia katika sehemu hiyo kuna kituo kikubwa kimoja (stendi ya daladala).