Mohammed Gulam Dewji

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

'

Mohammed Gulam Dewji
Dewji mwaka 2013
Amezaliwa8 Mei 1975
Kazi yakemfanyabiashara


Mohammed Gulam Dewji (maarufu kama "Mo"; amezaliwa tarehe 8 Mei 1975) ni mwekezaji na mfanyabiashara wa Tanzania aliyewahi kuwa mwanasiasa na mbunge katika Bunge la Tanzania miaka 2005-2015. Dewji aliwahi kuwa Mjumbe wa Bunge la Tanzania kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoka 2005 hadi 2015 kwa mji wake wa Singida.

Raisi mstaafu wa Tanzania, Mh. Jakaya Kikwete na Mohammed Dewji katika kampeni za uchaguzi za mwaka 2010.

Ukiachana na uanasiasa, ni miongoni mwa watu matajiri zaidi Afrika; kwa Tanzania ni wa kwanza katika utajiri.

Yeye ni mmiliki wa MeTL Group, iliyoanzishwa na baba yake miaka ya 1970. Mnamo Oktoba 2018, Dewji alikuwa na wastani wa jumla wa dola bilioni 1.5 za Kimarekani, kwa hivyo akamweka kama mtu tajiri wa 17 barani Afrika na bilionea kijana zaidi wa bara. Dewji pia ni Mtanzania wa kwanza kufunika jarida la Forbes mnamo 2013 akishika nafasi ya 1,500 kwa utajiri duniani

Kutekwa[hariri | hariri chanzo]

Tarehe 11 Oktoba 2018, saa 11:35 alfajiri, Dewji alitekwa na watu wenye silaha, nje ya Colosseum Hotel mjini Dar es Salaam, alipokwenda kufanya mazoezi.

Tarehe 15 Oktoba familia ilitangaza kuwa tayari kutoa shilingi bilioni moja kwa atakayetoa taarifa itakayosaidia kumpata hai mtoto wao.

Tarehe 20 Oktoba saa 8 usiku Dewji aliachwa huru katikati ya jiji la Dar es Salaam na watu wasiojulikana waliotumia gari lilelile lililotumika kumteka[1].

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]