Shilingi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Shilingi ya Scotland mnamo mwaka 1933

Shilingi ni pesa inayotumika kwa malipo halali katika nchi za Tanzania, Kenya, Uganda na Somalia.

Historia ya Shilingi

Asili ya jina ni kitengo cha kihistoria cha pesa katika nchi mbalimbali za Ulaya kama vile Austria, Uswisi, Uingereza, Poland, Denmaki, Norwei na Uswidi. Katika nchi nyingi kati ya hizo pesa hii haikutumika tena isipokuwa hadi mwaka 1971 Pauni 1 ya Kiingereza ilikuwa na shilling 12 na kila shilling ilikuwa na penny 20. Nchi nyingi zilizorithi mfumo wa pesa kutoka Uingereza walitumia pauni na shilingi hadi kuhamia kwenye pesa ya desimali.

Vilevile huko Austria "Schilling" ilikuwa pesa rasmi hadi kuhamia kwenye Euro.

Shilingi ya Afrika Mashariki

Uingereza ilitoa "East African Shilling" kuanzia mwaka 1921 kama pesa ya pamoja kwa ajili ya makoloni yake ya Kenya, Uganda na Tanganyika. Zanzibar ilijiunga na shilingi hiyo mwaka 1935 ilipoacha rupia zake.

Baada ya uhuru nchi hizo zilivunja umoja wa kifedha zikaanzisha pesa zao za pekee. Zote zinaitwa shilingi lakini thamani ilianza kutofautiana haraka.

Kuna majadiliano ya kurudisha shilingi ya pamoja kwa nchi za Jumuia ya Afrika ya Mashariki. Kwanza ilitarajiwa kuanzishwa mwaka 2012, halafu mwaka 2015, sasa mwaka 2024.

Picha

ThreeCoins.svg Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Shilingi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.