Rupia
Mandhari
Rupia ni jina la pesa inayotumika leo huko India na katika nchi mbalimbali za Asia.
Ni pia jina la pesa iliyowahi kutumika Afrika ya Mashariki na nchi mbalimbali.
Jina na historia
[hariri | hariri chanzo]Neno "rupia" limetokana na lugha ya Kihindi cha kale "rūp" au "rūpā" linalomaanisha "fedha". Katika lugha ya Sanskrit "rupyakam" (रूप्यकम्) inamaanisha sarafu ya fedha. Hii ni asili ya "Rūpaya" iliyotumika katika India kama sarafu yenye gramu 11.66 za fedha tangu mwaka 1540. Rupia moja ilikuwa na Anna 16, Paisa 64 au Pai 192.
Pesa ya kisasa
[hariri | hariri chanzo]Leo hii nchi zifuatazo zinatumia jina la Rupia (Rupiah, Rupee: ₨) kwa pesa zao:
Pesa ya kihistoria
[hariri | hariri chanzo]Rupia ilikuwa pesa ya nchi na maeneo yafuatayo:
- Afrika ya Mashariki ya Kijerumani (DOA) kwa jina la "Rupie ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani"
- Afrika ya Mashariki ya Kiingereza
- Zanzibar
- Kwenye eneo la India ya leo katika makoloni ya nchi zifuatazo: Denmark, Ufaransa na Ureno, pia katika madola mbalimbali ya Kihindi kabla ya ukoloni na kabla ya uhuru kama vile Hyderabad.
- Katika nchi jirani za India kama vile Bhutan, Burma, Sri Lanka, Afghanistan
- Katika maeneo ya Ghuba ya Uajemi
- Somalia ya Kiitalia
- Indonesia wakati wa uvamizi wa Japan (1940-1945)
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Rupie 1 ya Shirika la Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki, mbele (maandishi: Deutsch-Ostafrikanische Gesellschaft - Eine Rupie = Shirika la Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki - Rupia moja)
-
Rupie 1, nyuma (picha ya Kaisari Wilhelm II, maandishi ya Kilatini: Guilhelmus II Imperator)