Kaisari Wilhelm II

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Wilhelm II
Wilhelm II kwenye rupia ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani

Kaisari Wilhelm II (jina kamili: Friedrich Wilhelm Viktor Albert von Hohenzollern; 27 Januari 18594 Juni 1941) alikuwa mfalme wa mwisho wa Prussia na kaisari wa mwisho wa Ujerumani kuanzia mwaka 1888 hadi 1918.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Alizaliwa na mfalme mteule Friedrich III akiwa mjukuu wa Kaisari Wilhelm I. Baba yake alikufa baada ya utawala mfupi wa siku 99 pekee, hivyo Wilhelm II akawa mfalme na kaisari akiwa na umri wa miaka 29. Mwanzoni alitawala pamoja na chansella Otto von Bismarck lakini baada ya miezi michache alifarakana naye na kumwachisha.

Wilhelm alitaka kupatanisha wafanyakazi wa Ujerumani -waliofuata chama cha kisoshalisti- na utawala wa kifalme lakini hakuwa tayari kuongeza demokrasia. Alichukia bunge lililokataa mara kadhaa madai yake ya kupanua jeshi. Alipigania upanuzi wa jeshi la maji, uliojenga wasiwasi wa Uingereza juu ya uhusiano wake na Ujerumani.

Akiwa pia mkuu wa makoloni ya Ujerumani, kama vile Afrika ya Mashariki ya Kijerumani. Aliona koloni kama suala la heshima ya kitaifa, ilhali hakujali wenyeji na tamaduni zao.

Wataalamu wanaona ya kwamba alikuwa na jukumu kubwa kwa kutokea kwa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia.

Mwaka 1918, baada ya vita ya miaka minne, wafanyakazi na wanajeshi wa Ujerumani waligoma. Wilhelm pamoja na wafalme na makabaila wote wa Ujerumani walipinduliwa hata Ujerumani ilipata kuwa jamhuri. Wilhelm alihamia Uholanzi alipoishi hadi mwaka 1941. Hapo alikufa na kuzikwa kwa sababu hakutaka kuzikwa katika Ujerumani isiyo na utaratibu wa kifalme.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons