Chansella

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Chansella (kwa Kijerumani: "Kanzler") ni cheo cha mkuu wa serikali, lakini si mkuu wa dola, katika Ujerumani na Austria. Kinafanana na cheo cha waziri mkuu.

Vinginevyo neno hili limemaanisha vyeo mbalimbali vya ngazi tofauti. Asili ya neno ni Kilatini "cancellarius" la kumtaja mtu mwenye ofisi aliyewajibika kutoa vyeti rasmi. Wakati mwingine neno lilimtaja mwandishi tu. Lakini lilitumika pia kwa ajili ya cheo cha "Mwandishi Mkuu" kilichoweza kufanana na "Katibu Mkuu" kwa Kiswahili yaani msimamizi wa kazi ya utawala.

Katika nchi za Ujerumani na Austria ni cheo cha mkuu wa serikali. Uswisi linamaanisha Katibu Mkuu wa ofisi ya serikali.

Huko Uingereza chansella ni cheo cha waziri wa fedha ("Chancellor of the Exchequer") pia cheo cha afisa mkuu wa bunge ("Lord Chancellor") ambaye ni mwenyekiti wa nyumba ya juu bungeni.

Cheo cha chansella kinapatikana kimataifa pia kwenye vyuo vikuu vya nchi mbalimbali likimtaja ama mkuu wa chuo au mkuu wa utawala wa chuo. Katika nchi kadhaa za Afrika rais wa taifa amejipatia au kupatiwa cheo cha chansella wa chuo kikuu. Katika nchi hizi -jinsi ilivyokuwa nchini Kenya hadi mwaka 2003- mkuu halisi wa chuo alikuwa na cheo cha makamu wa chansella.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]