Kisanskrit

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Sanskrit)
Mwandiko wa Sanskrit

Sanskrit ni lugha ya kale ya Uhindi. Ni maarufu kama lugha ya vitabu vitakatifu vya Uhindu na Ubuddha.

Siku hizi ni lugha ya elimu na ya kidini inayojifunzwa na wataalamu na makuhani. Katika shule za sekondari nchini Uhindi inafundishwa pia na wanafunzi wengi wanapata kiwango fulani cha lugha hii. Zamani ilijadiliwa na watu kama lugha ya kawaida. Tangu karne kadhaa huandikwa kwa mwandiko wa Devanagari.

Sanskrit imepangwa pamoja na Kihindi na Kiurdu kati ya Lugha za Kihindi-Kiarya ambazo ni kitengo cha Lugha za Kihindi-Kiajemi ndani ya familia ya lugha za Kihindi-Kiulaya.

Wikipedia
Wikipedia
Kisanskrit ni toleo la Wikipedia, kamusi elezo huru

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kisanskrit kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.