Viktoria wa Uingereza

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Malkia Viktoria

Malkia Viktoria wa Uingereza (24 Mei 181922 Januari 1901) alikuwa malkia wa Ufalme wa Muungano wa Britania na Ueire tangu 1837 hadi 1901. Hadi sasa (2008) hakuna mfalme au malkia mwingine aliyeshika nafasi ya mkuu wa dola kwa muda mrefu zaidi.

Alipewa hadhi ya malkia kwa umri wa miaka 18. Mjomba wake William IV alikuwa mfalme na wakati alipofariki amekuwa mrithi kwa sababu babaye alikuwa ameshaaga dunia.

Alipokuwa malkia tayari Uingereza ilikuwa tayari ufalme wa kikatiba na madaraka ya mfalme au malkia yameshapungua. Lakini aliheshimiwa sana akawa ishara ya maendeleo na enzi ya Uingereza. Wakati wake nchi iliendelea kuwa nchi yenye nguvu duniani na kujenga utawala juu ya koloni nyingi. Mapinduzi ya viwanda yalifika kilele chake na Uingereza ilishinda nchi zote za dunia kiteknolojia, kiuchumi na kijeshi. Kwenye mwisho wa utawala wake uwezo huu umeshapungua kutokana na manedeleo katika nchi kama Ujerumani na Marekani lakini alisimamia milki iliyounganisha theluthi moja ya watu wote duniani sehemu ya tanuo (20%) ya uso wa dunia.

Kipindi chake huitwa mara nyingi "enzi ya Viktoria".

Mwaka 1840 alimwoa Albert wa Saksonia-Coburg na Gotha akazaa naye watoto 9. Albert aliaga dunia mapema mwaka 1861 akiwa na miaka 42 pekee na Viktoria aliendelea kuonyesha huzuni yake akaendelea kuvaa nguo za mjane kwa miaka mingi iliyofuata.

Wakati Uingereza ilipopanusha utawala wake duniani alipewa pia cheo cha kaisari cha Uhindi. Binti yake wa kwanza aliolewa na Kaisari Wilhelm II wa Ujerumani.

Kipindi chake kilikuwa kipindi cha maendeleo ya kiuchumi na matabaka ya juu na ya kati yaliona manedeleo makubwa maishani lakini matabaka ya chini bado yalikuwa na maisha magumu. Hata kama jeshi la Uingereza ilipigania vita vingi duniani katika koloni zake watu wa Uingereza penyewe waliona kipindi kirefu cha amani na maendeleo.