Jakaya Kikwete

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jakaya Mrisho Kikwete


Muda wa Utawala
21 Disemba 2005 – 5 Novemba 2015
Makamu wa Rais Ali M. Shein (2005–2010)
Mohamed Bilal (2010–2015)
Waziri Mkuu Edward Lowassa (2005–08)
Mizengo Pinda (2008–2015)
mtangulizi Benjamin Mkapa
aliyemfuata John Magufuli

Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika
Muda wa Utawala
31 Januari 2008 – 2 Februari 2009
mtangulizi John Kufuor
aliyemfuata Muammar al-Gaddafi

Muda wa Utawala
Novemba 1995 – 21 Disemba 2005
Rais Benjamin Mkapa
aliyemfuata Asha-Rose Migiro

Muda wa Utawala
1994 – 1995
mtangulizi Steven Kibona
aliyemfuata Simon Mbilinyi

Mbunge wa Tanzania
wa jimbo la Chalinze
Muda wa Utawala
Novemba 1995 – 2005
aliyemfuata Ramadhani Maneno

tarehe ya kuzaliwa 7 Oktoba 1950 (1950-10-07) (umri 73)
Msoga, Tanganyika
utaifa Mtanzania
chama CCM
chamakingine TANU
ndoa Salma Kikwete
watoto 8
makazi Ikulu, Dar es Salaam
mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Fani yake Mchumi
dini Uislamu
Military service
Allegiance Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Service/branch Jeshi la Tanzania
Rank Major
Rais Kikwete pamoja na marais wastaafu Mwinyi na Mkapa
Kikwete alikuwa rais wa kwanza kutoka barani Afrika kukutana na Rais Barack Obama mwaka 2009.
Rais Kikwete na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakifurahia jambo
KATIKA picha:
1. Mlangoni: Jakaya Kikwete
2. Mama mtumzima: Mamake Kikwete
3. Aliyekumbatiwa na mama mtumzima: Ridhiwani Kikwete
4. Anayefuatia: Salama Kikwete
5. Babu: Baba mzazi wa rais mstaafu Jakaya Kikwete.
Historia ya Tanzania
Coat of Arms of Tanzania
This article is part of a series
Uendo
Historia ya Zanzibar
Afrika Mashariki 1800-1845
Ukoloni
Afrika ya Mashariki ya Kijerumani
Mkataba wa Zanzibar-Helgoland
Mkwawa
Vita vya Maji Maji
Vita vikuu vya kwanza Afrika Mashariki
Tanganyika
Mapambano ya uhuru Tanganyika
Uhuru
Uhuru wa Tanganyika
Mapinduzi ya Zanzibar
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
Julius Nyerere
Ujamaa
Tamko la Arusha
Vita vya Kagera
Ali Hassan Mwinyi
Benjamin Mkapa
Jakaya Kikwete
John Magufuli
Samia Suluhu Hassan

Tanzania Portal

Jakaya Mrisho Kikwete alikuwa rais wa nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tangu tarehe 21 Desemba 2005 hadi tarehe 5 Novemba 2015.

Asili

Amezaliwa 7 Oktoba 1950 katika kijiji cha Msoga, kata ya Lugoba, tarafa ya Msoga, jimbo la uchaguzi la Chalinze, Wilaya ya Bagamoyo, mkoa wa Pwani.

Lugha ya mama ilikuwa Kikwere.

Alizaliwa katika familia ya wanasiasa. Babu yake Mzee Mrisho Kikwete alikuwa chifu wa Wakwere. Baba yake alikuwa Mkuu wa Wilaya Pangani, Same na Tanga.

Jakaya Kikwete amesimulia hadithi ya kifamilia ya kuwa wakati mama yake alipokuwa mja mzito naye, babu alitamka kuwa ikiwa mtoto atakuwa wa kiume atampatia urithi wa cheo chake.

Masomo

Miaka 19581961 akasoma Shule ya Msingi Msoga, halafu 19621965 Shule ya Kati (Middle School) Lusonga, halafu Shule ya Sekondari Kibaha akiongeza A-level huko Shule ya Sekondari Tanga.

Kuanzia mwaka 1972 alisoma uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akimaliza kwa kupata digrii yake mwaka 1978.

Akajiunga na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Jakaya aliposoma Shule ya Sekondari ya Kibaha alikuwa mwenyekiti wa wanafunzi na pia wa Vijana wa TANU. Katika Shule ya Sekondari Tanga alikuwa Kiranja Mkuu na pia kiongozi wa timu ya mpira. Katika UDS alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa halmashauri ya wanafunzi.

Kupanda ngazi katika siasa

1mwaka huu alikuwa mkulima wa Msoga. Mwaka 1988 akateuliwa kuwa mbunge na waziri msaidizi. Mwaka 1990 alichaguliwa kuwa mbunge wa Bagamoyo/Chalinze akirudishwa kila uchaguzi hadi mwaka 2000. Akawa waziri akipita katika wizara za maji na fedha.

Mwaka 1995 alijaribu kuchaguliwa kuwa mgombea wa urais upande wa CCM. Inasemekana ya kwamba Mwalimu Julius Nyerere alimwomba wakati ule kumwachia nafasi Benjamin Mkapa aliyeteuliwa na Halmashauri Kuu ya CCM. Kikwete akawa Waziri wa Mambo ya Nje katika serikali zote mbili za Mkapa.

Mwaka 2005 alifaulu kuteuliwa mgombea wa CCM kwa nafasi ya rais akashinda uchaguzi wa Desemba 2005 akizoa 80% za kura zote.

Miaka kumi ya urais

Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 alitangazwa tena mshindi ingawa kwa asilimia ndogo zaidi na kwa wasiwasi kuhusu uwezekano wa matokeo kuchakachuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi aliyoiteua mwenyewe. Katiba ya nchi hairuhusu kukata rufaa dhidi ya tangazo la tume hiyo.

Kuapishwa kwa mara ya kwanza kwa Jakaya Kikwete kama Rais wa 4 wa Tanzania kulifanyika Jumatano, tarehe 21 Desemba 2005. Ilikuwa ni mwanzo wa muhula wa kwanza wa miaka mitano wa Jakaya Kikwete kama Rais na Ali Mohamed Shein kama Makamu wa Rais.

Katika miaka mitano iliyofuata, rais aliendelea kusafiri sana nje ya nchi, kiasi kwamba alikaa ughaibuni siku nyingi kuliko zile alizokaa nchini Tanzania.

Hali ya mwisho ya nchi ilifananishwa na mwandamizi wake John Magufuli kuwa kama "shamba la bibi", ambamo kila mtu anaweza kuchuma anavyotaka. Pia rais mpya alilalamika kwa kukuta hazina haina fedha, mbali na madeni ya kimataifa kufikia kiasi cha karibu Shilingi za Tanzania milioni 1 kwa kila mwananchi.

Heshima na Tuzo

Nishani

Nishani Nchi Tarehe Ref
Nishani Ubora wa Lulu ya Afrika (Bwana tukufu) Bendera ya Uganda Uganda Julai 2007 [1]
Nishani ya Hilali Kijani ya Komori Bendera ya Komori Komori Machi 2009 [2]
Nishani ya Abdulaziz Al Saud Bendera ya Saudi Arabia Saudi Arabia Aprili 2009 [3]
Nishani ya Ubora Bendera ya Jamaika Jamaika Novemba 2009 [4]
Nishani ya Oman (Daraja la Kwanza) Bendera ya Omani Omani Oktoba 2012 [5]

Shahada za Heshima

Chuo Kikuu Nchi Shahada ya Uzamivu Tarehe Ref
Chuo Kikuu cha Mtakatifu Thomas (Minnesota) Marekani Daktari wa Sheria 28 Septemba 2006 [6][7]
Chuo Kikuu cha Kenyatta Bendera ya Kenya Kenya Shahada ya Heshima 19 Disemba 2008 [8]
Chuo Kikuu cha Fatih Uturuki Shahada ya Heshima katika Mahusiano wa Kimataifa Februari 2010 [9]
Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Muhimbili Bendera ya Tanzania Tanzania Daktari wa Afya ya Umma Disemba 2010 [10]
Chuo Kikuu cha Dodoma Bendera ya Tanzania Tanzania Shahada ya Heshima 26 Novemba 2010 [11]
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Bendera ya Tanzania Tanzania Daktari wa Sheria Oktoba 2011 [12]
Chuo Kikuu cha Guelph Bendera ya Kanada Kanada Daktari wa Sheria 20 Septemba 2013 [13][14]
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Bendera ya Tanzania Tanzania Shahada ya Heshima 21 Januari 2016 [15]

Marejeo

  • Nyang'oro, Julius E. (2011). JK: A Political Biography of Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania. Trenton, NJ: Africa World Press, Inc. ISBN 1592217753. 

Tanbihi

  1. "Museveni honours Nyerere", 10 July 2007. Retrieved on 26 Septemba 2013. (Kiingereza) Archived from the original on 2014-12-05. 
  2. Rais Kikwete, Jenerali Mwamunyange, Waziri Membe Watunukiwa Anjoun. Ikulu (25 March 2009). Jalada kutoka ya awali juu ya 2013-09-27. Iliwekwa mnamo 26 Septemba 2013.
  3. JK akiwa Saudia. Michuzi Blog (16 April 2009). Iliwekwa mnamo 26 Septemba 2013.
  4. "President Kikwete Awarded Order of Excellence", 26 November 2009. Retrieved on 26 Septemba 2013. (Kiingereza) Archived from the original on 2013-09-27. 
  5. "HM confers Oman Civil Order on Tanzania leader", October 2012. Retrieved on 26 Septemba 2013. (Kiingereza) Archived from the original on 2014-12-04. 
  6. President of Tanzania to speak here Sept. 28 (Kiingereza). Chuo Kikuu cha Mtakatifu Thomas (Minnesota) (25 September 2006). Jalada kutoka ya awali juu ya 2013-09-28. Iliwekwa mnamo 25 Septemba 2013.
  7. Swallehe Msuya. "Tanzania's president touts country's progress at St. Thomas appearance", 30 September 2006. Retrieved on 25 Septemba 2013. (Kiingereza) 
  8. Kenyatta University Newsletter Vol. 4, Issue 15 (Special Graduation Edition) (PDF) (Kiingereza). Chuo Kikuu cha Kenyatta (26 January 2009). Jalada kutoka ya awali juu ya 2017-04-21. Iliwekwa mnamo 25 Septemba 2013.
  9. (in Kiingereza) Honorary Doctorate to the president of Tanzania from our university (Press release). Turkey: Chuo Kikuu cha Fatih. 19 February 2010. Archived from the original on 2012-12-24. https://web.archive.org/web/20121224011640/http://fatih.edu.tr/?basin_bultenleri%2C12&language=EN. Retrieved 25 Septemba 2013.
  10. MUHAS Annual Report 2010-2011 (PDF) (Kiingereza). Chuo Kikuu cha Muhimbili (2011). Jalada kutoka ya awali juu ya 2013-09-30. Iliwekwa mnamo 25 Septemba 2013.
  11. "JK, late Kawawa honoured at UDOM colourful, maiden graduation", 27 November 2010. Retrieved on 25 Septemba 2013. (Kiingereza) 
  12. JK atunukiwa udaktari wa sheria UDSM (Kiingereza). Michuzi Blog (21 Ocotober 2011). Iliwekwa mnamo 25 Septemba 2013.
  13. (in Kiingereza) U of G to Welcome Tanzanian President to Campus (Press release). Guelph, Canada: Chuo Kikuu cha Guelph. 18 September 2013. http://www.uoguelph.ca/news/2013/09/u_of_g_to_welcome_tanzanian_president.html. Retrieved 25 Septemba 2013.
  14. President of Tanzania at War Memorial Hall katika YouTube
  15. Rais Mstaafu Jakaya Kikwete atunukiwa shahada ya udaktari ya uhusiano wa kimataifa (Kiswahili) (21 Januari 2016). Iliwekwa mnamo 1 Agosti 2020.

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Alitanguliwa na
Benjamin William Mkapa
Rais wa Tanzania
2005-2015
Akafuatiwa na
John Magufuli