Uendo wa historia ya Tanzania

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Historia ya Tanzania
Coat of Arms of Tanzania
This article is part of a series
Uendo
Historia ya Zanzibar
Afrika Mashariki 1800-1845
Ukoloni
Afrika ya Mashariki ya Kijerumani
Mkataba wa Zanzibar-Helgoland
Mkwawa
Vita vya Maji Maji
Vita vikuu vya kwanza Afrika Mashariki
Tanganyika
Mapambano ya uhuru Tanganyika
Uhuru
Uhuru wa Tanganyika
Mapinduzi ya Zanzibar
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
Julius Nyerere
Ujamaa
Tamko la Arusha
Vita vya Kagera
Ali Hassan Mwinyi
Benjamin Mkapa
Jakaya Kikwete
John Magufuli
Samia Suluhu Hassan

Tanzania Portal

Uendo wa historia ya Tanzania unaeleza mfululizo wa matukio makubwa yanayohusu wananchi wa Tanzania, ikiwa ni pamoja na Zanzibar, na eneo la zamani la Tanganyika na maeneo yanayoizunguka Tanzania kabla ya ukoloni wa Kizungu.

Ushahidi wa kiakiolojia unaonesha uwepo wa sokwe watu katika kanda hii kwa zaidi ya miaka milioni 3 iliyopita na Paranthropus kwa zaidi ya miaka milioni 2 iliyopita.

Makazi ya watu katika kanda yalianza angalau miaka 100,000 iliyopita. Wakhoisan wanadhaniwa kuhamia maeneo haya wakiwa kama wawindaji tu walau miaka 10,000 iliyopita.

Mawasiliano ya Wazungu katika Afrika ya Mashariki yalifanywa mnamo karne ya 15 na mpelelezi wa Ureno, Vasco da Gama. Aliwasili mjini Kilimane (sasa hivi Tanzania) kunako mwaka wa 1498.

Zanzibar, funguvisiwa vilivyopo majini mashariki kwa Tanzania bara, vilichukuliwa na Dola la Ureno likabaki kuwa eneo lake kwa takriban miaka 200 hivi.

Baadaye eneo lile likachukuliwa na Sultani wa Oman mnamo 1698.

Hekaheka za ukoloni zilipamba moto katika kanda hii kunako karne ya 19.

Afrika ya Mashariki ya Kijerumani ilianzishwa Tanzania bara mnamo 1885 na Zanzibar ikawa chini ya udhibiti wa Uingereza mnamo 1890.

Miaka sita baadaye, Vita ya Zanzibar na Uingereza ilipigwa kisiwani humo, moja kati ya vita vifupi mno katika historia.

Chifu Mkwawa wa kabila la Wahehe na wapiganaji wake walipinga utawala wa kikoloni katika Afrika ya Mashariki ya Kijerumani.

Mfano wao ulifuatwa baadaye na kikosi kizima cha makabila ya kusini katika Vita ya Maji Maji.

Hekaheka za Kijerumani ziliisha baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia wakati Uingereza ulichukua Tanganyika kwa mamlaka ya Shirikisho la Mataifa.

Vikundi vya kijamii na kisiasa vilianza kazi ya kuhamasisha watu katikati ya karne ya 20.

Mwaka 1961 mwalimu wa shule wa zamani Julius Nyerere akawa Waziri Mkuu wa kwanza.

Tanganyika ikapata uhuru wake mwaka 1962, na Nyerere akawa ndiye rais wa kwanza mwaka uliofuata.

Uhuru wa Zanzibar kutoka kwa Waingereza ukapatikana mwaka uliofuata, halafu wananchi wakamfukuza sultani.

Mataifa hayo mawili yaliungana mnamo 1964 na kuwa nchi inayojulikana kama Tanzania.

Nyerere aliongoza nchi kwa chama kimoja kwa zaidi ya miaka 20, huku akitambulisha maoni yake juu ya Usoshalisti wa Kiafrika, Ujamaa.

Aliachia ngazi mnamo 1985 akafuatiwa na Ali Hassan Mwinyi.

Benjamin Mkapa, rais wa awamu ya tatu nchini, alishinda uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi Tanzania mnamo 1995. Wakati wa urais wa Mkapa, Tanzania iligushi uhusiano wa kidiplomasia katika kanda kwa kusaini Mkataba wa Jumuia ya Afrika Mashariki.

Mwaka wa 1998, Ubalozi wa Marekani ulishambuliwa kwa bomu mjini Dar es Salaam.

Mwaka wa 2003, jenasi mpya ya ngedere imegunduliwa nchini, ya kwanza kugunduliwa tangu mwaka wa 1923.

Rais Jakaya Kikwete alichaguliwa mnamo 2005 na kuongoza hadi 2015, alipomuachia John Pombe Magufuli.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]