Nenda kwa yaliyomo

Benjamin Mkapa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Benjamin Mkapa


Muda wa Utawala
23 Novemba 1995 – 21 Decemba 2005
Makamu wa Rais Omar Ali Juma (1995–2001)
Ali Mohamed Shein (2001-05)
mtangulizi Ali Hassan Mwinyi
aliyemfuata Jakaya Kikwete

Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu,
Muda wa Utawala
1992 – 1995
Rais Ali Hassan Mwinyi

Waziri wa Habari na Utangazaji
Muda wa Utawala
1990 – 1992
Rais Ali Hassan Mwinyi

tarehe ya kuzaliwa (1938-11-12)12 Novemba 1938
Ndanda, Masasi, Tanganyika
tarehe ya kufa 24 Julai 2020
Dar es Salaam
utaifa Mtanzania
chama CCM
ndoa Anna Mkapa
watoto 2
mhitimu wa Chuo Kikuu cha Makerere
Chuo Kikuu cha Columbia
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania
Fani yake mwandishi wa habari, mwanadiplomasia
dini Ukristo (Kanisa Katoliki)
Historia ya Tanzania
Coat of Arms of Tanzania
This article is part of a series
Uendo
Historia ya Zanzibar
Afrika Mashariki 1800-1845
Ukoloni
Afrika ya Mashariki ya Kijerumani
Mkataba wa Zanzibar-Helgoland
Mkwawa
Vita vya Maji Maji
Vita vikuu vya kwanza Afrika Mashariki
Tanganyika
Mapambano ya uhuru Tanganyika
Uhuru
Uhuru wa Tanganyika
Mapinduzi ya Zanzibar
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
Julius Nyerere
Ujamaa
Tamko la Arusha
Vita vya Kagera
Ali Hassan Mwinyi
Benjamin Mkapa
Jakaya Kikwete
John Magufuli
Samia Suluhu Hassan

Tanzania Portal

Benjamini William Mkapa (12 Novemba 1938 - 24 Julai 2020) alikuwa Rais wa awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1995-2005) na mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, CCM.[1]

Wasifu

Mkapa alizaliwa Lupaso karibu na Masasi katika kusini-mashariki ya Tanganyika. Kuanzia 1945 hadi 1951 alsoma shule za msingi pale Lupaso na Ndanda. 1952/53 alisoma shule ya seminari ya Kigonsera akaendelea kwenye shule ya sekondari ya watawa Wabenedikto pale Ndanda hadi kumaliza O-level. 1958/59 alimaliza A-levels pale St Farncis, Dar es Salaam (leo hii Pugu Secondary). Alipokelewa kwenye Chuo Kikuu cha Makerere alipohitimu 1962. [2]

Hatua za maisha ya kazi[3]

  • Aprili 1962: Afisa tawala Dodoma
  • Aprili 1962: Mkuu wa Wilaya
  • Agosti 1962: alijiunga na Utumishi wa wizara ya mambo ya nje
  • Mei 1966: Mhariri mkuu, gazeti la Uhuru
  • Aprili 1972: Mhariri mkuu, Daily News
  • Julai 1974: Afisa habari katika Ofisi ya Rais, Dar es Salaam
  • Julai 1976: Mwanzilishi na mhariri mkuu wa Shirika la habari la Tanzania (SHIHATA)
  • Oktoba 1976: Balozi wa Tanzania pale Nigeria
  • Februari 1977: Waziri wa Mambo ya Wje
  • Novemba 1980: Waziri wa Habari na Utamaduni
  • Aprili 1982: Balozi wa Tanzania pale Kanada
  • Februari 1983: Balozi wa Tanzania pale Marekani
  • Aprili 1984: Waziri wa Mambo ya Nje
  • 1990: Waziri wa Habari na Utangazaji
  • Mei 1992: Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu
  • Novemba 1995: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Rais wa Tanzania

Katika mwaka wa 1995, Mkapa alichaguliwa rais msingi wake ukiwa kampeni maarufu ya kupambana na ufisadi na kuuungwa mkono kwa nguvu na rais wa zamani Julius Nyerere [4]. Juhudi za Mkapa za kupambana na ufisadi ni pamoja na kuumba jukwaa la wazi lililoitwa Tume ya Rais juu ya Ufisadi (Tume ya Warioba) na kuongeza msaada kwa Afisi ya Kuzuia Ufisadi.[4]

Muhula wa pili wa miaka 5 wa Mkapa kama Rais uliisha Desemba 2005. Katika wakati wake ofisini, Mkapa alibinafsisha kampuni zilizomilikiwa na serikali akaweka sera za soko huria.[5] Wafuasi wake walimtetea kuwa kuvutia uwekezaji wa kigeni ungesaidia kukuza uchumi. Sera zake zilipata msaada wa Benki ya Dunia na IMF na kupelekea baadhi ya madeni ya nje ya Tanzania kufutiliwa mbali.[4]

Amekashifiwa kwa upungufu wa baadhi ya jitihada zake za kupambana na ufisadi [4] vilevile matumizi mabaya ya fedha za umma. Utawala wake ulikuwa na matumizi sana na maposho bila kikomo. Alitumia £ 15 milioni kununua ndege ya binafsi ya kirais, vilevile karibu £ 30 milioni kwa vifaa vya angani vya kijeshi ambavyo wataalamu waliona yalizidi mahitaji machache ya majeshi ya nchi.[6] Ilikuwa juu ya ununuzi huo wa mwisho ndipo katibu wa maendeleo ya kimataifa wa Uingereza wa wakati huo Clare Short alielezea hasira ya umma, na kusababisha yeye kujulikana kama 'Mama Radar' katika vyombo vya habari vya Tanzania.

Baada ya kutoka ofisini kwa kukamilisha mihula miwili inayoruhusiwa, Mkapa alikumbwa na shutuma nyingi za ufisadi kati yao kujipa mwenyewe na Waziri wake wa zamani wa nishati na madini Daniel Yona "Mgodi wa Makaa ya Mawe wa Kiwira" yenye faida kubwa katika Nyanda za juu za kusini mwa Tanzania bila taratibu zifuatazo. Kwa kujibinafsishia mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira, alivunja katiba ya Tanzania ambayo haimruhusu rais kufanya biashara yoyote katika ikulu[onesha uthibitisho].

Aliteuliwa katika Bodi ya Wadhamini ya Chuo cha Aga Khan mwezi Novemba 2007.[5]

Heshima na Tuzo

Nishani

Nishani Nchi Mwaka Ref
Nishani ya Moyo wa Dhahabu wa Kenya (Chifu) Bendera ya Kenya Kenya 2005 [7]
Nishani ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Bendera ya Tanzania Tanzania 2011

Mnamo Desemba 7, 2019, alitunukiwa Nishani ya Heshima ikiwa ni kuthamini mchango wake katika kuanzisha vyuo vikuu binafsi, hivyo kukifanya Chuo Kikuu cha Iringa kuwa chuo kikuu cha kwanza binafsi nchini Tanzania wakati wa utawala wake.

Shahada za Heshima

Chuo Kikuu Nchi Shahada ya Uzamivu Mwaka Ref
Chuo Kikuu cha Sōka Bendera ya Japani Japan Shahada ya Heshima 1998 [8]
Chuo cha Morehouse Marekani Shahada ya Heshima 1999 [8]
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Bendera ya Tanzania Tanzania Shahada ya Heshima 2003 [8]
Chuo Kikuu ya Kitaifa cha Lesotho Bendera ya Lesotho Lesotho Daktari wa Sheria 2005 [8]
Chuo Kikuu cha Kenyatta Bendera ya Kenya Kenya Daktari wa Elimu 2005 [9]
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Bendera ya Tanzania Tanzania Shahada ya Heshima 2005 [8]
Chuo Kikuu cha Nyukasal Ufalme wa Muungano Daktari wa Sheria ya Kiraia 2007 [10]
Chuo Kikuu cha Rasi ya Pwani (Cape Coast) Bendera ya Ghana Ghana Daktari wa Barua 2008 [11]
Chuo Kikuu cha Makerere
Bendera ya Uganda Uganda Daktari wa Sheria 2009 [12]

Marejeo

  1. "Benjamin Mkapa", Microsoft Encarta Encyclopedia 2001, WGBH (FM), pbs.org, ilitolewa 19-Oktoba-2009
  2. "Benjamin Mkapa,". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-01-06. Iliwekwa mnamo 2010-01-17.
  3. ABOUT President of Tanzania BENJAMIN WILLIAM MKAPA, tovuti ya dsctanzia.org ya 2004, sehemu ya tovuti ya Delray Beach Sister Cities' programme, ilivyohifadhiwa kwenye archive.org, kuangaliwa Agosti 2020
  4. 4.0 4.1 4.2 4.3 Bruce Heilman na Laurean Ndumbaro, "Corruption, Politics and Societal Values in Tanzania: An Evaluation of the Mkapa Administration's Anti-Corruption Efforts", Afr. J. polit. sd. (2002), Toleo 1 Nambari 7
  5. 5.0 5.1 "Mheshimiwa Benjamin William Mkapa", Ilihifadhiwa 3 Septemba 2011 kwenye Wayback Machine. Bodi ya Wadhamini, Chuo cha AKU, ilitolewa 19-10-2009
  6. Gideoni Burrows, "We sell arms to Saddam's friends", New Statesman, 8 Septemba 2003
  7. "Mkapa lauds Kenya's democratic posture". panapress.com. 12 Oktoba 2005. Iliwekwa mnamo 26 Septemba 2013. {{cite web}}: Italic or bold markup not allowed in: |publisher= (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  8. 8.0 8.1 8.2 8.3 8.4 "83RD Annual District Conference & Assembly" (PDF) (kwa Kiingereza). Page 10, Rotary International District 9200. 17 Mei 2008. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2013-06-25. Iliwekwa mnamo 26 Septemba 2013.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  9. "Prominent Alumni" (kwa Kiingereza). Kenyatta University. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-09-30. Iliwekwa mnamo 26 Septemba 2013.
  10. "Citation: Benjamin William Mkapa DCL" (PDF) (kwa Kiingereza). Newcastle University. 2007. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2013-05-31. Iliwekwa mnamo 26 Septemba 2013.
  11. "UCC honours former Tanzanian leader". modernghana.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 26 Septemba 2013.
  12. "H.E. Benjamin Mkapa receives Makerere Honorary PhD" (kwa Kiingereza). Makerere University. 27 Novemba 2009. Iliwekwa mnamo 26 Septemba 2013.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

Viungo vya nje

Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu:
Alitanguliwa na
Ali Hassan Mwinyi
Rais wa Tanzania
1995-2005
Akafuatiwa na
Jakaya Kikwete
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Benjamin Mkapa kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.