Nenda kwa yaliyomo

Jiografia ya Tanzania

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ramani ya zamani ya Tanzania kiutawala.
Pwani ya Tanzania kutoka juu.
Milima ya Usambara.
Milima ya Uluguru.

Jiografia ya Tanzania inahusu nchi hiyo ambayo ina historia yake kuu ni uhuru na muungano. Kabla ya kuitwa Tanzania nchi upande wa bara iliitwa Tanganyika na ilipata uhuru tarehe 9 Desemba 1961. Baada ya uhuru wa funguvisiwa la Zanzibar, ilijihusisha katika muungano wa nchi mbili ambazo ni Tanganyika na Zanzibar zilizoungana mnamo 26 Aprili 1964 kuunda TanZanIa.

Tanzania ni nchi iliyomo mashariki mwa Afrika. Nchi hiyo inazungukwa na bahari upande wa mashariki, Kenya na Uganda upande wa kaskazini, Malawi upande wa kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo upande wa magharibi.

Tanzania ina eneo la takriban km2 947.303.

Nchi iko katika eneo la Maziwa makubwa ya Afrika, hivyo maziwa yanafunika km2 61,500, yaani 6% za eneo lote la nchi.

Pia ina mito mingi ambayo inaelekeza maji yake katika Bahari ya Hindi mashariki mwa nchi, lakini mingine inachangia Mto Zambezi kupitia Ziwa Nyasa, michache Bahari ya Kati kupitia Ziwa Victoria na mto Naili, mingine tena Bahari Atlantiki kupitia Ziwa Tanganyika na mingine inaishia katika mabonde kama ya Ziwa Rukwa.

Karibu thuluthi moja ya nchi inalindwa kwa namna moja au nyingine: kuna Hifadhi za Taifa 16, mbali ya Hifadhi Teule, Hifadhi za Mawindo, Mapori ya Akiba n.k.

Tanzania ni mojawapo ya nchi zenye vivutio mbalimbali vya watalii kutoka maeneo mengi duniani. Vivutio hivyo ni kama vile milima, mbuga za wanyama, kumbukumbu za maisha ya watu wa kale n.k. Tanzania imebahatika kuwa na kivutio kikubwa Duniani ambacho ni Mlima Kilimanjaro, mmojawapo kati ya milima mikubwa na mirefu duniani. Mlima Kilimanjaro una urefu wa zaidi ya futi 5300 kutokea ardhini. Mlima huo unapatikana katika Mkoa wa Kilimanjaro.

Mbali na mlima huo wa Kilimanjaro, Tanzania inayo milima mingine kama vile Milima ya Uluguru, Milima ya Udzungwa, Mlima Oldonyo Lengai n.k.

Tabianchi

[hariri | hariri chanzo]

Tabia ya nchi ya Tanzania hubadilika kwa nyakati tofautitofauti katika mwaka.

Hivyo kiasi cha mvua na halijoto husababisha tofauti za aina ya uoto wa asili, udongo na aina ya mazao yanayolimwa.

Tanzania ina idadi kubwa sana ya watu waishio nchini, kutokana na makabila mbalimbali yaliyomo nchini, yakiwemo ya Wasukuma, Wanyamwezi, Wahaya, Waha, Wagogo, Wanyakyusa, Wahehe, Wachaga, Waluguru, Wazaramo na mengineyo.

Watu waishio nchini ni wa dini tofauti wakiwemo Waislamu (31.4%) na Wakristo (35.5%) kadiri ya sensa ya miaka ya 1960.

Mpaka sasa muungano umekuwa na marais wanaume watano: Julius Kambarage Nyerere, Benjamin William Mkapa, Ali Hassan Mwinyi, Jakaya Mrisho Kikwete, John Pombe Magufuli, wa sita akiwa Samia Suluhu Hassan, mwanamke.

Mji mkuu

[hariri | hariri chanzo]

Mji mkuu wa Tanzania ni jiji la Dodoma.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]