Tabianchi ya Tanzania

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Tabia ya nchi Tanzania)
Ramani ya Tanzania.
Ramani ya Tanzania.
Mahali pa Tanzania.
Aina za tabianchi katika Tanzania kadiri ya Köppen.
Tanzania kutoka angani.
Topografia ya Tanzania.

Tabianchi ni hali ya mabadiliko ya mazingira upande wa hali ya hewa yaani halijoto, pepo zinazovuma na mvua ambayo yanayojirudia rudia kwa muda mrefu.

Tanzania ni nchi iliyopo mashariki mwa bara la Afrika na imepakana na nchi zifuatazo: upande wa kaskazini imepakana na nchi za Kenya na Uganda, upande wa magharibi imepakana na nchi za Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, upande wa kusini kuna nchi za Zambia, Malawi na Msumbiji wakati upande wa mashariki kuna Bahari ya Hindi.

Tabianchi ya Tanzania hubadilika kwa nyakati tofautitofauti katika mwaka.

Hivyo kiasi cha mvua na halijoto husababisha tofauti za aina ya uoto wa asili, udongo na aina ya mazao yanayolimwa.

Mabadiliko ya tabianchi duniani kote yanajitokeza Tanzania pia. Kwa mfano, ongezeko la joto Duniani linasababisha barafuto la mlima Kilimanjaro kuzidi kuyeyuka. Serikali ya nchi imeungana na zile za nchi nyingi kukabili tatizo hilo lakini Kigezo:Bajeti iliyopangwa ni ndogo.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Vitabu vya Jiografia ya Tanzania

Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.