Kupanda kwa halijoto duniani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Mabadiliko ya halijoto duniani katika karne zilizopita; makadirio 10 ya kisayansi yameunganishwa hapa. Yale ya zamani yana rangi ya buluu, yale ya kisasa yana rangi nyekundu; nyekundu kali ni kadirio la mwisho.

Kupanda kwa halijoto duniani (ing. global warming) ni mchakato wa mabadiliko ya tabianchi yaliyotambuliwa na wataalamu tangu miaka kadhaa.

Mchakato huo ulianza pamoja na usambazaji wa viwanda duniani. Unaonekana kwa kulinganisha vipimo vya halijoto vinavyopatikana tangu miaka 150. Kupanda huku kunaleta mabadiliko ya hali ya hewa yaliyoanza tayari kuathiri maisha ya watu na uhai kwa ujumla.

Kuna hofu ya kwamba mabadiliko hayo yataleta hatari kubwa kwa jamii.

Kati ya wanasayansi kuna tofauti ya maoni kama sababu za mabadiliko hayo ni shughuli za binadamu tu au kama kuna sababu asilia. Siku hizi wataalamu wengi wanafikiri ya kwamba sababu kuu ni kuchoma kwa makaa na mafuta katika viwanda, magari na vituo vya umeme kunakopuliza hewani gesijoto kama dioksidi kabonia.

Vipimo na data

Duniani kuna upimaji wa kisayansi wa halijoto tangu mwaka 1860. Kabla ya hapo kuna kumbukumbu ya hali ya hewa katika karne zilizopita kutoka mahali mbalimbali ambazo hazikusanifishwa wakati ule.

Leo hii wanasayansi wanatumia vipimo na taarifa za kale wakipiga makadirio juu ya hali ya hewa katika historia.

Hapo wanatumia pia mbinu kama kulinganisha miviringo kwenye mashina ya miti inayoonyesha miaka yenye mvua nyingi au kidogo au wanapima kiwango cha dioksidi kabonia kwenye barafu ya chini nchani yenye umri wa miaka 10,000 na zaidi.

Makadirio ya hali ya hewa hutofautiana, lakini kwa jumla kuna picha juu ya miaka 1,000 iliyopita. Watalaamu wanakubaliana ya kwamba mnamo mwaka 1000 kulikuwa na kipindi cha joto kiasi, tena kipindi cha baridi kiasi kuanzia mnamo mwaka 1600.

Lakini hakuna hakika bado juu ya athira duniani kwa sababu sehemu kubwa ya data ni kutoka upande wa kaskazini ya dunia.

Vipimo vya kisayansi vinavyopatikana vinaonyesha ya kwamba halijoto ya wastani duniani imepanda sentigredi 0.7 kati ya 1906 na 2005. Hii si kiwango kidogo; wakati wa zama za barafu kubwa miaka 100,000 iliyopita halijoto ilikuwa tu 6 °C chini ya wastani ya leo na hii ilitosha kufunika sehemu kubwa za Ulaya, Asia na Amerika ya Kaskazini kwa mabapa manene ya barafu.

Dalili zote zinadokeza ya kwamba kupanda kwa halijoto kuliharakishwa tangu mwaka 1970 na kunaelekea kupanda zaidi.

Sababu za kuongezeka kwa halijoto

Kwa miaka kadhaa wataalamu hawakukubaliana juu ya sababu za kuongezeka kwa halijoto. Kwa jumla kuna maelezo mawili tofauti:

  • Kupanda kwa halijoto ni jambo la kawaida lenye sababu asilia; historia inaonyesha vipindi vya joto na vipindi vya baridi na sababu kuu ni mabadiliko ya kiwango cha mnururisho wa jua unaofika duniani. Mabadiliko hayo hayakueleweka bado, lakini labda kuna kitu kama majira ya jua yenyewe yanayobadilika kila baada ya miaka mia kadhaa.
  • Kupanda kwa halijoto kwa sasa si jambo la kawaida kwa sababu kunaenda sambamba na kuongezeka kwa gesi kama dioksidi kabonia hewani kutokana na shughuli za binadamu hasa kuchoma makaa na mafuta ya petroli.

Siku hizi wataalamu wengi wanaelekea upande wa pili maana wanaona mbali na sababu asilia kuna athira za kibinadamu zinazobadilisha hali ya hewa.

Matokeo yanayotazamiwa

Wataalamu wanaonya ya kwamba kupanda kwa halijoto kunaweza kuleta mabadiliko kama yafuatayo:

Juhudi za kimataifa

Kutokana na hatari zinazotazamiwa na karibu wataalamu wote wa elimu ya tabianchi duniani Umoja wa Mataifa ulifanya jitihada za kuanzisha hatua za kisiasa za kupambana na hatari hizi. Tokeo lake ni Kongamano la Mfumo wa UM kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (en:United Nations Framework Convention on Climate Change) ya mwaka 1993 ambayo nchi 194 zilijiunga nayo.

Nchi wanachama ziliendelea kupatana hatua mbalimbali katika miniti za Kyoto na Mapatano ya Paris kuhusu Tabianchi ya mwaka 2015 ambayo nchi wanachama ziliahidi kuchukua hatua maalumu ya kupakana kupanda kwa halijoto kwa kiwango chini ya sentigredi 2 kwa wastani.

Tazama pia

Viungo vya nje

Vipimo na data

Suala la dioksidi kabonia

Tovuti za kisayansi

Habari za ziada

Mengine