Mapatano ya Paris kuhusu Tabianchi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nchi wanachama wa Mapatano ya Paris      Waliotiha sahihi na kuikubali kufuatana na sheria ya kila nchi      waliotia sahihi tu

Mapatano ya Paris kuhusu Tabianchi (en:Paris Agreement, fr:Accord de Paris) ni mapatano yaliyokubaliwa mwaka 2015 mjini Paris (Ufaransa) kufuatana na Kongamano la Mfumo wa UM kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi.

Hadi Mei 2017 nchi 197 zilitia sahihi ambazo ni sawa na wanachama wote wa UM isipokuwa Syria na Nikaragua, lakini tarehe 1 Juni 2017 rais Donald Trump wa Marekani alitangaza ya kwamba anataka kutoka katika mapatano hayo.[1]

Shabaha[hariri | hariri chanzo]

Nchi wanachama zilipatana kuhusu shabaha zifuatazo:

"(a) Kupatana ongezeko la halijoto ya wastani duniani kwenye kiwango chini ya sentigredi 2 ya wastani ya kipindi kabla ya mapinduzi ya viwandani na kulenga mpaka wa ongezeko la halijoto kwa 1.5°C juu ya kiwango kabla ya viwanda, kwa kutambua ya kwamba hii itapunguza hatari ya mabadiliko ya tabianchi.

(b) Kuimarisha uwezo wa kupatana na athari hatari za mabadiliko ya tabianchi na kujenga unyumbukaji dhidi ya mabadiliko hayo na kupunguza ongezeko la gesijoto kwa njia zisizohatarisha uzalishaji wa vyakula.

(c) Kupatanisha sera ya fedha na mwelekeo wa kupunguza gesijoto na maendeleo yenye unyumbufu dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.

Njia[hariri | hariri chanzo]

Kila nchi inatakiwa kupanga siasa yake ipasavyo na kuchukua hatua halisi na kutoa taarifa kuhusu hatua hizi kwa ofisi ya UNFCCC na nchi nyingine.

Lakini mapatano hayana masharti ya kisheria, hivyo kila nchi inachangia kwa hiari yake.

Matokeo[hariri | hariri chanzo]

Nchi nyingi zilileta taarifa ya kwamba zilibadilisha sheria na maagizo kwa ajili ya uchumi wao. Unyumbufu dhidi ya mabadiliko ya tabianchi unadai mabadiliko kama vile

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

  1. Trump on Paris accord: 'We're getting out', tovuti ya CNN tar 1 Juni 2017