Gesijoto

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Hesabu ya viwango vya joto vinavyopoelewa na dunia, kuakisishwa angani na kuzunguka katika angahewa

Gesijoto (ing.Greenhouse gases) ni aina za gesi katika angahewa ya dunia zenye uwezo wa kuathiri mnururisho wa infraredi yaani wa joto. Ni sababu muhimu ya kupanda kwa halijoto duniani.

Kazi ya gesijoto[hariri | hariri chanzo]

Gesijoto zinarudisha sehemu ya joto inayotoka ardhini kuelekea anga la nje na kuirudisha ardhini.

Kuna gesijoto asilia na pia gesijoto zilizosababishwa na binadamu. Kuwepo kwa gesijoto si jambo baya maana binadamu na maumbile asilia yote vilitokea katika dunia penye gesijoto. Gesijoto zinaunda uwezo wa angahewa ya dunia kutunza joto. Bila gesijoto asilia dunia yetu ingekuwa baridi mno, kwa wastani na sentigredi -18 °C badala ya wastani ya +14 °C jinsi ilivyo sasa.

Kwa hiyo kama kiwango cha gesi hizi kinapanda kuna tokeo ya kwamba pia halijoto ya dunia inapanda kwa sababu upotevu wa kawaida wa joto kutoka dunia kwenda angani unapungua.

Tatizo linalojadiliwa tangu miaka 20 hivi ni mabadiliko ya kiasi cha gesijoto katika angahewa yaliyosababishwa na shughuli za kibinadamu. Kuongezeka kwa gesijoto hewani kunasababisha kupanda kwa halijoto duniani kunakoleta hasara kwa spishi nyingi.

Aina za gesijoto[hariri | hariri chanzo]

Gesijoto asilia zinazopatikana katika angahewa na kutunza joto la sayari ni pamoja na mvuke wa maji, hewa ukaa (kaboni dioksidi), methani, oksidi dinitrojeni (N2O) na ozoni O2

Matatizo ya kuongezeka kwa gesijoto zinazosababishwa na binadamu[hariri | hariri chanzo]

Tatizo ni kupanda kwa halijoto katika miaka 150 iliyopita kutokana na shughuli za kibinadamu zilizosababisha kuongezeka kwa gesijoto juu ya kiwango asilia. Shughuli hizi kama kuchoma makaa mawe na mafuta ya petroli zilisababisha kuongezeka kwa gesijoto zinzopelekwa angahewa. Zilianza kuwa muhimu tangu vyanzo vya viwanda na mashine zinazoendeshwa kwa fueli kisukuu katika karne ya 19.

Kati ya gesijoto zilizoongezeka tangu karne ya 19 ni hasa gesi ya ukaa (kaboni dioksidi).

Pamoja na kuchoma fueli kisukuu njia nyingine ya kuongeza gesi ya ukaa ni kukata miti kwa wingi. Miti ina tabia ya kujenga miili yao kwa kutoa gesi ya ukaa hewani.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]