Orodha ya makabila ya Tanzania
Makala hii inahitaji vyanzo zaidi ili kuwezesha kuonyesha uthibitisho. |
Orodha ya makabila ya Tanzania inayotolewa hapa inataja makabila zaidi ya mia moja na ishirini (120) ambayo hupatikana katika mikoa yote ya Tanzania. Ni orodha ya makabila ya watu ambao wamekuwa wanaishi tangu zamani katika eneo ambalo sasa linaitwa Tanzania, pamoja na makabila yaliyogawiwa na mipaka baina ya Tanzania na nchi za jirani. Orodha hii haizingatii makabila yanayoishi katika Tanzania kama wakimbizi tu, hasa kutokana na vita katika nchi za jirani. Vilevile ukurasa huu hauorodheshi vikundi vya wahamiaji kutoka nchi za kigeni, kama wahamiaji au wazao wao kutoka Uarabuni au Uhindi.
Juu ya hiyo, hakuna ufafanuzi wa wazi kusema kikundi fulani ni kabila au siyo. Vikundi kadhaa katika orodha hii vina wenyeji mamia tu, lakini vikundi vingine vina mamilioni ya watu; labda kila kikundi kinaitwa "kabila," lakini ni jamii za aina tofauti kabisa. Vikundi katika ukurasa huu vimeorodheshwa kuwa vikundi tofauti kutokana na ushahidi wa kutofautisha lugha zao unaotokana na orodha ya lugha za Tanzania inayopatikana katika Ethnologue [1] pamoja na tovuti nyingine [2]; inaweza kuwa na matatizo kwenye majina kadhaa, kwa sababu mbalimbali. Kwa mfano, inawezekana kwamba baadhi ya majina ya makabila ni majina ya lugha au lahaja tu, badala ya makabila, na labda majina mengine yaliandikwa vibaya.
Orodha
- Waakie
- Waakiek
- Waalagwa (pia: Wasi)
- Waarusha
- Waassa
- Wabarabaig (pia: Wamang'ati)
- Wabembe
- Wabena
- Wabende
- Wabondei
- Wabungu (au Wawungu)
- Waburunge
- Wachagga
- Wadatoga
- Wadhaiso
- Wadigo
- Wadoe
- Wafipa
- Wagogo
- Wagoma
- Wagorowa (pia: Wafiome)
- Wagweno
- Waha
- Wahadzabe (pia: Wahadza na Watindiga)
- Wahangaza
- Wahaya
- Wahehe
- Wahinda
- Wahutu
- Waikizu
- Waikoma
- Wairaqw (pia: Wambulu)
- Waisanzu
- Waissenye
- Wajaluo
- Wajiji
- Wajita
- Wakabwa
- Wakaguru
- Wakahe
- Wakami
- Wakara (pia: Waregi)
- Wakerewe
- Wakimbu
- Wakinga
- Wakisankasa
- Wakisi
- Wakonongo
- Wakuria
- Wakutu
- Wakw'adza
- Wakwavi
- Wakwaya
- Wakwere (pia: Wanghwele)
- Wakwifa
- Walambya
- Walongo
- Waluguru
- Walungu
- Wamachinga
- Wamagoma
- Wamahanji
- Wamakonde
- Wamakua (au: Wamakhuwa)
- Wamakwe (pia: Wamaraba)
- Wamalila
- Wamambwe
- Wamanda
- Wamanyema
- Wamasai
- Wamatengo
- Wamatumbi
- Wamaviha
- Wambugwe
- Wambunga
- Wameru
- Wamosiro
- Wampoto
- Wamwera
- Wandali
- Wandamba
- Wandendeule
- Wandengereko
- Wandonde
- Wanena
- Wangasa
- Wangindo
- Wangoni
- Wangulu
- Wangurimi (au: Wangoreme)
- Wanilamba (au: Wanyiramba)
- Wanindi
- Wanyakyusa
- Wanyambo
- Wanyamwanga
- Wanyamwezi
- Wanyanyembe
- Wanyasa
- Wanyaturu (pia: Warimi)
- Wanyiha
- Waokiek
- Wapangwa
- Wapare (pia: Wasu)
- Wapimbwe
- Wapogolo
- Warangi (au: Walangi)
- Warufiji
- Warungi
- Warungu (au: Walungu)
- Warungwa
- Warwa
- Wasafwa
- Wasagara
- Wasandawe
- Wasangu (Tanzania)
- Wasegeju
- Washambaa
- Washirazi
- Washubi
- Wasizaki
- Wasuba
- Wasukuma
- Wasumbwa
- Waswahili
- Wataveta
- Watemi (pia: Wasonjo)
- Watongwe
- Watumbuka
- Wavidunda
- Wavinza
- Wawanda
- Wawanji
- Waware (lugha yao imekufa)
- Wayao
- Wazanaki
- Wazaramo
- Wazigula
- Wazinza
- Wazyoba