Nenda kwa yaliyomo

Waikizu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Waikizu ni watu wa kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Mara. Lugha yao ni Kiikizu: lugha hiyo inafanana sana na lugha ya Wazanaki na Wakurya na asili ya lugha hizi tatu ni moja, ila kuna tofauti ndogo za lahaja.

Kabila hilo linapatikana hasa katika wilaya ya Bunda, eneo maarufu linaloitwa Ikizu.

Watu wa jamii hiyo hujihusisha na shughuli za kilimo na ufugaji ingawa pia uwindaji ulikuwa ukifanyika enzi za kale katika mbuga za wanyama. Zao kuu la biashara ni pamba na zao la chakula ni mahindi pamoja na mihogo (ugali wa udaga).

Waikizu ni watu jasiri sana na watu ambao wanajali sana mila zao na kulinda utamaduni wao dhidi ya mabadiliko mbalimbali yanayotokea katika mazingira. Moja ya sifa nyingine za Waikizu ni uvumilivu.

Kuna watu maarufu kama waziri mkuu wa zamani wa Tanzania, ndugu Joseph Sinde Warioba.

Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Waikizu kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.