Wameru (Tanzania)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kabila la Wameru huishi pembezoni mwa mlima Meru.

Wameru wa Tanzania (au "Warwa") ni kabila la watu wa Kibantu wa jamii ya Wachaga wanaoishi hasa kwenye Mlima Meru katika Mkoa wa Arusha, kaskazini mwa nchi ya Tanzania.

Lugha yao ni Kirwa[1].

Wanakadiriwa kuwa milioni 2, wengi wao wakifuata dini ya Ukristo.

Mbali na jina, Wameru hao ni tofauti kabisa na Wameru wa Kenya kwa historia na utambulisho. Sanasana ni kwamba pande zote mbili ni wakulima wenye bidii kubwa[2].

Inasemekana Wameru walifikia mlima huo miaka 800 hivi iliyopita wakitokea milima ya Usambara, Mkoa wa Tanga. Walikuta huko wawindaji walioitwa Wakoningo ambao walikuja kumezwa na jamii ya Wameru.[3]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. [1]
  2. Fosbrooke, Henry. waMeru People. Arusha Integrated Regional Development Plan 5. Iliwekwa mnamo 2016-09-17.
  3. HISTORIA YA WAMERU.. ONLINE TUITION. Iliwekwa mnamo 2024-01-13.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Taarifa nyingi kuwahusu Warwa (Wameru) zinapatikana katika kitabu kiitwacho "Mountain Farmers-Moral Economies of Land & Agricultural Development in Arusha & Meru" kilichoandikwa na Prof. Thomas T. Spear.

Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wameru (Tanzania) kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.