Wambugwe
Mandhari
Wambugwe (au Vambowe) ni kabila la watu wa Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Manyara na hata katika mkoa wa Arusha. Wanapatikana hasa kaskazini mwa wilaya ya Babati, Tarafa ya Mbugwe katika Bonde la Ufa la Afrika Mashariki.
Kabila la Wambugwe ni wa jamii ya Wabantu na inasemekana walitokana na Warangi. Lugha yao ni Kimbugwe na inafanana na Kirangi.
Mwaka 1999 walikadiriwa kuwa 24,000. Wengi wao ni wafugaji na wakulima.
Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Wambugwe kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |