Warungwa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Warungwa ni kabila la watu kutoka eneo la wilaya ya Mpanda, mkoa wa Katavi, magharibi mwa nchi ya Tanzania. Mwaka 1987 idadi ya Warungwa ilikadiriwa kuwa 18,000.

Lugha yao ni Kirungwa [1].

Ni dhahiri kuwa Warungwa waliishi eneo/kijiji kilichoitwa Rungwa ambapo walipapenda, hasa kutokana na shughuli zao, kwani wao shughuli zao kubwa ni kilimo, ufugaji, uvuvi na uwindaji wa wanyamapori.

Eneo la Rungwa kwa sasa lipo ndani ya hifadhi ya Katavi baada ya kuwaondoa wakazi wa eneo hilo mwaka 1974, kipindi cha operesheni vijijini na mpaka sasa jamii ya Warungwa inapatikana katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Katavi kama vile: Kasansa, Majimoto, Mamba, Inyonga, Mpanda, Sitalike, Mpimbwe na sehemu nyingine ambapo walikwenda kwa lengo la kuendeleza shughuli zao za maisha.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Warungwa kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.