Hifadhi ya Katavi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Vipoko

Hifadhi ya Katavi ni moja ya hifadhi za taifa ambayo iko juu ya uwanda mpana wa mafuriko magharibi mwa Tanzania katika mkoa wa Rukwa. Ina ukubwa wa eneo la kilometa za mraba 4471.

Mandhari kuu katika hifadhi[hariri | hariri chanzo]

  • Maeneo ya majimaji yenye majani
  • Mimea jamii ya mitende na
  • Mto Katuma

Hifadhi hii inasifika kwa:

  • Idadi kubwa ya mamba na viboko

Pia wanyama kama simba na chui hawana shida ya mawindo kwani katika himaya yao kuna makundi ya swala, nyamela topi wa miguu mieupe, pundamilia na nyati.

Kuna ainazipatazo 400 za ndege waliozagaa katika miti ya acacia, kingo za mto, mabwawa na makundi kadhaa ya mwari(pelicans) yanayoambaa ziwani. Nikawaida kuyaona makundi makubwa ya tembo yalkila majani katika mabwawa huku miili yao ikiwa imefunikwa na maji na magugu.

Namna ya kufikaa katika hifadhi[hariri | hariri chanzo]

  • Inafikika kwa ndege kutoka miji ya Dar es salaam na Arusha
  • Kwa gari kutoka mji wa Mbeya au kupitia mji wa Kigoma

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Majarida ya hifadhi za Taifa Tanzania


Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]