Waha

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Waha ni kabila la watu wa Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Kigoma, pia mpakani kwa Burundi.

Lugha yao ni Kiha

Kabila la Waha limetokana na mtawanyiko wa makabila ya Warundi na Wahaya, kipindi cha kuhamahama kwa ajili ya kutafuta masilahi kama vile chakula na kukimbia vita. Baada ya kufika kando ya ziwa Tanganyika na maeneo yote yanayolizunguka Ziwa Tanganyika waliweza kukaa na kuanzisha shughuli mbalimbali kama vile kilimo, uvuvi, ufugaji na uwindaji.

Waha walipoanza kuyazoea mazingira, walijigamba na kujidai kwa makundi ya kikoo kuwa yana nguvu, kila mmoja kwa nafasi yake. Kila ukoo ulijigamba kwa kutumia majina ya wanyama, wadudu, ndege, milima n.k.

Kwa mfano, kuna waliokuwa wakijigamba kuwa wao ni Washubi ambao walijulikana kwa mnyama ambaye ni kondoo yaani kuwa wapole, sisimizi (chunguchungu)

Walijigamba kama wakulima, wengine kama konoo, kiboko, n.k. na walijulikana tabia zao kulingana na majina ya koo zao.

Kilimo cha Waha ni mahindi, maharage, ndizi, kahawa, mhogo, karanga, mbaazi, njegere, viazi mviringo, viazi vitamu, mtama, ulezi, mahore, miwa, mpunga, korosho n.k.

Pia Waha ni wavuvi wa samaki katika ziwa Tanganyika, mto Malagarasi, Mto Rwiche, Mto Mkoza, na mito mingine midogomidogo kama vile, Nyajijima, Mresi, Kazingu, n.k.

Waha ni wafugaji wa ng'ombe, mbuzi, kuku, bata, nguruwe, sungura, mbwa, paka, n.k.

Biashara zao ni mazao wanayoyalima, samaki, na bidhaa nyingine za kawaida.

Usafiri wao wa asili ulikuwa wa miguu yao wenyewe, ambapo kuna imani ilikuwepo pia ya kusadikika kuwa walitumia ungo kusafiria kama ndege yao ya asili.

Utamaduni wao, yaani mavazi yao ilikuwa ni magome ya miti yaliyojulikana kama mpuzu, na nyumba zao ni za msonge, udongo na miti, kulingana na sehemu mbalimbali, maana kuna sehemu zenye joto kama vile bondeni, na sehemu zenye baridi kama vile nyanda za juu.