Mkoa wa Kigoma

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Mkoa wa Kigoma katika Tanzania

Kigoma iko kati ya mikoa 26 za Tanzania. Imepakana na Burundi na Mkoa wa Kagera upande wa Kaskazini, mikoa ya Shinyanga na Tabora upande wa mashariki na Mkoa wa Rukwa upande wa kusini. Magharibi umepakana na Ziwa la Tanganyika penye mpaka na Kongo.

Eneo la Mkoa[hariri | hariri chanzo]

Mkoa una eneo la 45,066 km² (sawa na 4.8% ya eneo lote la Tanzania) ikiwa 8,029 km² ndizo maji hasa Ziwa la Tanganyika na 37,037 km² ndizo nchi kavu.

Wilaya au manisipaa Eneo km² Wakazi Kata
1 Buhigwe 9,324 120,690 15
2 Kakonko 9,324 81,417 11
3 Kasulu Mjini 2,128 208,244 9
4 Kasulu Vijijini 7,196 207,421 19
4 Kibondo 16,058 125,284 13
4 Kigoma - Ujiji 93 215,458 19
4 Kigoma Vijijini 968 101,499 11
4 Uvinza 9,324 189,130 14
Jumla 45,066 2.127.930 121

Mnamo Machi 2012 zimeongezwa wilaya mpya za Buhigwe, Kakonko na Uvinza.

Takriban robo ya eneo la mkoa wa Kigoma hutumika kwa kilimo na ufugaji, karibu nusu ni misitu.

Kwa ujumla eneo la mkoa ni tambarare ya juu inayoanza kwenye UB wa 800m karibu na Ziwa Tanganyika na kupanda hadi mita 1,750.

Mito ya kudumu ndiyo Malagarasi, Luiche na Ruchugi.

Utawala[hariri | hariri chanzo]

Kuna wilaya nne ndizo (idadi ya wakazi katika mabano): Kigoma Mjini (144,852), Kigoma Vijijini (490,816), Kibondo (414,764) na Kasulu (628,677). Jumla ya wakazi ni 1,679,109 (sensa 2002). Makao makuu ndipo Kigoma mjini.


Wakazi[hariri | hariri chanzo]

Kabila kubwa ni Waha,Wabembe na Wamanyema. Kuna pia Wabembe, Wanyamwezi, Wasukuma, Wafipa na watu wenye asili ya Kongo, Rwanda na Burundi.

Idadi au msongamano wa watu katika maeneo ya mkoa huu imetegemea sana kupatikana kwa nzi aina ya ndorobo: penye ndorobo wengi watu ni wachache.

Uchumi na mawasiliano[hariri | hariri chanzo]

Mkoa wa Kigoma haukuona bado maendeleo yanayolingana na mazingira yake. Hali ya barabara na mawasiliano mengine ni mbaya. Umbali hadi Daressalaam ni 1316 km, hadi Mwanza 830 Km, hadi Arusha 1204 Km. Lakini hakuna barabara ya lami hata barabara za kokoto ni sehemu ndogo to.

Usafiri muhimu ni reli ya kati kutoka Kigoma kwenda Daressalaam kupitia Tabora na Dodoma. Isipokuwa reli hii imeshazeeka ilhali imejengwa zamani za Afrika ya Mashariki ya Kijerumani kabla ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Treni zake huchelewachelewa zinachukua muda mrefu. Wakati wa mvua inatokea ya kwamba mawasiliano yanavurugika.

Uwanja wa ndege wa Kigoma inashughulika ndege ndogo aina ya Fokker.

Mnamo 85% ya wakazi wote hutegema kilimo, walio wengi kilimo cha kujitegemea tu.

Kuongezeka kwa wakimbizi kutoka nchi jirani na kukua kwa makambi kulikuwa tatizo kubwa.

Hifadhi za wanyama na za kihistoria[hariri | hariri chanzo]

Kuna maeneo mawili penye sokwe: ndipo Hifadhi ya Taifa ya Gombe (alikofanya utafiti wake mwanabiolojia Jane Goddall) na Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale.

Mji wa Ujiji ulioko karibu na Kigoma mjini ndio mji wa kale zaidi katika Tanzania ya Magharibi penye makumbusho wa Dr. Livingstone.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]


 
Mikoa ya Tanzania
Bandera Tanzania
Arusha | Dar es Salaam | Dodoma | Geita | Iringa | Kagera | Katavi | Kigoma | Kilimanjaro | Lindi | Manyara | Mara | Mbeya | Morogoro | Mtwara | Mwanza | Njombe | Pemba Kaskazini | Pemba Kusini | Pwani | Rukwa | Ruvuma | Shinyanga | Simiyu | Singida | Tabora | Tanga | Unguja Kaskazini | Unguja Kusini | Unguja Mjini Magharibi