Nenda kwa yaliyomo

Chama cha Demokrasia na Maendeleo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Chadema)

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (kifupi: Chadema) ni chama cha kisiasa nchini Tanzania ambacho kuanzia mwaka 2010 kilikuwa chama kikuu cha upinzani.

Kilianzishwa tarehe 28 Mei 1992 na mwanasiasa mkongwe Edwin Mtei, aliyewahi kuwa waziri wa fedha katika miaka 1977 hadi 1979.

Mwaka 2000 chama cha Chadema hakikuwa na mgombea wa urais. Mwaka 2005 mgombea wa Chadema Freeman Mbowe alikuwa namba tatu kati ya wagombea kumi akapata asilimia 5.88 za kura.

Mwaka 2010 Chadema ilipata asilimia 27.1% na mgombea urais wa chama Wilbrod Peter Slaa na kura 4,627,923 kwa 31.75%.

Mwaka 2015 mgombea wa Chadema alikuwa Edward Ngoyai Lowassa aliyehama CCM na kuhamia Chadema baada ya kukatwa jina lake na kamati kuu ya CCM. Magufuli alipata kura 8,882,935, sawa na asilimia 58.46 na Lowassa alipata kura 6,072,848, sawa na asilimia 39.97.

Hata hivyo Chadema imekataa matokeo mengi kutokana na mchakato mzima kuwa mikononi mwa Tume ya Uchaguzi isiyo huru.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]