Bunge la Tanzania

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Bunge la Taifa la Tanzania)
Wabunge wa Bunge la 11 (2022), bila wabunge walioteuliwa na rais
*      CCM (363)
*      CHADEMA (20)
*      ACT (4)
*      CUF (3)
*      Mwanasheria Mkuu (1)


Bunge la Tanzania ni baraza la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linalotunga sheria na kuisimamia serikali katika utekelezaji wa majukumu yake.

Waliopo bungeni

Bunge linamjumuisha rais wa Tanzania pamoja na wabunge. Mnamo mwaka 2017 kulikuwa na wabunge 393[1] wanaoingia kwa namna tofauti [2]

Mamlaka ya Bunge iko juu ya mambo yote yasiyo ya Zanzibar pekee.

Majimbo ya Uchaguzi wa Bunge

Kuna majimbo 214 Tanzania Bara na majimbo 50 Zanzibar.

Majimbo yanatofautiana kwa kiasi kikubwa katika idadi ya wakazi. Wastani wa Tanzania bara ni mbunge mmoja kwa wakazi 227,461. [3] Kuna majimbo katika mikoa ambako mbunge mmoja anawakilisha watu wengi zaidi kama vile Dar es Salaam (wakazi 546,542/mbunge 1), Mwanza (346,999) na Kagera (309,953). Kinyume chake kuna majimbo mengine ambako mbunge anawakilisha watu wachache kama vile Pwani (wakazi 133.104/mbunge), Katavi (128.513), Njombe (120.795) au Lindi (112.192).

Tofauti ni kubwa zaidi huko Zanzibar. Kwa mfano Wilaya ya Kaskazini B katika Mkoa wa Unguja Kaskazini ina wakazi 81,675[4] pekee lakini inachagua wabunge 4 katika majimbo ya Bumbwini, Donge, Kiwengwa na Mahonda.

Kamati za Bunge

Bunge linatekeleza kazi yake kwa kiasi kikubwa kupitia kamati mbalimbali. Kuna aina tofauti za kama kama vile:

Kamati za kudumu zinazohusu uendeshaji wa Bunge:

  1. Kamati ya Uongozi;
  2. Kamati ya Kanuni za Bunge
  3. Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge.

Kamati za kudumu za Bunge za Kisekta

  1. Kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira
  2. Kamati ya Katiba na Sheria
  3. Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama;
  4. Kamati ya Utawala na Serikali za Mitaa;
  5. Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii
  6. Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii;
  7. Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji;
  8. Kamati ya Miundombinu;
  9. Kamati ya Nishati na Madini.

Kamati za Sekta Mtambuka:

  1. Kamati ya Bajeti
  2. Kamati ya Masuala ya UKIMWI;
  3. Kamati ya Sheria Ndogo;
  4. Kamati ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma.

Kamati za kudumu za Bunge zinazosimamia matumizi ya fedha za Umma:

  1. Kamati ya Hesabu za Serikali (Public Accounts Committee PAC)
  2. Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC)

Tazama pia

Tanbihi

  1. Structure of parliament, tovuti ya bunge, ilitazamiwa Mei 2017
  2. Katiba ya Tanzania Archived 16 Mei 2017 at the Wayback Machine., ibara 66, uk. 51
  3. Linganisha takwimu hii, hasa Jedwali 1 uk. 2: Makadirio ya idadi ya watu katika majimbo ya uchaguzi Tanzania Bara kwa mwaka 2016; tovuti ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu, iliangaliwa Juni 2017. Wastani unapatikana kwa kugawa idadi ya wakazi jumla kwa idadi ya majimbo
  4. Sensa ya 2012, Kaskazini Unguja uk. 226