Mwanasheria Mkuu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Mwanasheria Mkuu ni mtaalamu wa sheria mwenye kazi ya kushauri serikali au mahakama katika utekelezaji wa majukumu yake.

Nafasi hii inapatikana katika nchi mbalimbali hasa kama zinazothiriwa na haki ya Uingereza yaani katika koloni zake za zamani.

Anaweza kuchaguliwa na bunge, na rais au kamati za pekee.

Tanzania[hariri | hariri chanzo]

Nchini Tanzania mwanasheria mkuu anashiriki katika mikutano ya baraza la mawaziri, kazi yake ni kuwa mshauri mkuu wa serikali katika masuala ya kisheria, kuwakilisha na kutetea serikali mahakamani au hata kutoa shauri la kisheria kwa mahakimu.

Mwanasheria mkuu wa Tanzania anateuliwa na rais tu. Anaweza kuwa mbunge kutokana na wahifadhi wake na atashika madaraka yake mpaka uteuzi wake utakapofutwa na rais au mara tu kabla ya rais mteule kushika madaraka.