Baraza la Wawakilishi wa Zanzibar
Jump to navigation
Jump to search
Baraza la Wawakilishi wa Zanzibar ni bunge la Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ambayo ni sehemu ya Tanzania inayojitawala katika mambo mengi ya ndani.[1]
Historia[hariri | hariri chanzo]
Baraza ilianzishwa mwaka 1980. Kabla ya mwaka huu, Baraza la Mapinduzi lilikuwa na shughuli za serikali na pia bunge kwa muda wa miaka 16 baada ya Mapinduzi ya Zanzibar ya 1964.[2]
Wabunge wa baraza[hariri | hariri chanzo]
Baraza ina wabunge wafuatao:[1]
Aina ya mbunge | CCM | CUF | Jumla |
---|---|---|---|
Waliochaguliwa katika majimbo ya uchaguzi | 28 | 22 | 50 |
Walioteuliwa na Rais wa Zanzibar | 8 | 2 | 10 |
Viti maalum vya wanawake (% 40) | 11 | 9 | 20 |
Spika (kama si mbunge) | 1 | – | 1 |
Mwanasheria Mkuu (anaingia kwa cheo chake) | – | – | 1 |
Jumla | 48 | 33 | 82 |
Matokeo ya chaguzi za awali[hariri | hariri chanzo]
Tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi kulikuwa na matokeo yafuatayo:[3]
Chama | Mwaka wa uchaguzi | |||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|
1995 | 2000 | 2005 | ||||||
Chama Cha Mapinduzi (CCM) | 26 | 34 | 30 | |||||
Civic United Front (CUF) | 24 | 16 | 19 | |||||
Jumla | 50 | 50 | 50 |
Tazama pia[hariri | hariri chanzo]
Marejeo[hariri | hariri chanzo]
- ↑ 1.0 1.1 The Parliament of Zanzibar, Tanzania. Commonwealth Parliamentary Association. Jalada kutoka ya awali juu ya 2018-04-28. Iliwekwa mnamo 14 November 2014.
- ↑ History of the ZHoR. Zanzibar House of Representatives. Iliwekwa mnamo 15 November 2014.
- ↑ Elections in Zanzibar. Iliwekwa mnamo 15 November 2014.