Edward Ngoyai Lowassa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Edward Ngoyai Lowassa
Edward Lowasa (cropped).jpg
Mbunge
Bunge la Tanzania
Jimbo la uchaguzi Monduli (Arusha)
Tarehe ya kuzaliwa 26 Agosti 1953
Chama CHADEMA (tangu 28/07/15)
Tar. ya kuingia bunge tangu 1990
Alirudishwa mwaka 2005
Waziri Mkuu wa Tanzania
Alingia ofisini 2005
Alitanguliwa na Frederick Sumaye
Dini Mkristo
Elimu yake Chuo Kikuu
Digrii anazoshika MA (Development Studies) University of Bath (Uing.)
Kazi mwanasiasa

Edward Ngoyayi Lowassa (amezaliwa 26 Agosti 1953) ni mwanasiasa nchini Tanzania.

Alichaguliwa kuwa Waziri Mkuu wa kumi wa nchi hiyo tarehe 30 Desemba 2005 akajiuzulu tarehe 7 Februari 2008 kwa kashifa ya Richmond. Sasa ni mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Lowassa ni mwenyeji na alikuwa mbunge wa Monduli katika Mkoa wa Arusha.

Alisoma shahada ya kwanza katika mada ya tamthilia kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, halafu shahada ya pili katika sayansi ya maendeleo ya jamii kwenye Chuo Kikuu cha Hull nchini (Uingereza).

Mnamo tarehe 28 Julai 2015 alijunga rasmi na chama cha upinzani cha CHADEMA. Hiyo ni baada ya kukatwa jina lake katika kinyang'anyiro cha Urais kupitia chama tawala cha Chama cha Mapinduzi.

Siku chache baadaye aliteuliwa kuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya CHADEMA mnamo Oktoba 2015.

Nyadhifa mbalimbali alizowahi kushika[hariri | hariri chanzo]

Lowassa ni mwanasiasa mkongwe mwenye uzoefu mbalimbali katika siasa za nchini Tanzania, kwa kuwa aliwahi kushika vyeo mbalimbali katika serikali kama vile:

  • Waziri mdogo wa mazingira na mapambano dhidi ya umaskini katika ofisi ya Makamu wa Rais (1988-2000)
  • Mkurugenzi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (1989-1990)
  • Waziri mdogo wa haki na mambo ya bunge katika ofisi ya Makamu wa Rais (1990-1993)
  • Mbunge wa Monduli tangu 1990

Sakata la Richmond[hariri | hariri chanzo]

Sakata la Richmond lilianza kwa kuunda tume ya kuchunguza mchakato wa zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura: tume hiyo ilidai kampuni ya Richmond ilikuwa kampuni ya mfukoni, jambo ambalo inawezekana lina ukweli, maana hata kabla ya tume kuundwa Lowassa[onesha uthibitisho] alipata shaka na kampuni hiyo pale iliposuasua kutekeleza mradi akawa ameshauri mkataba na kampuni hiyo uvunjwe, lakini ushauri wa mtaalamu na wanasheria ulitaka serikali ivumilie.

Tume ilidai viongozi wa serikali wa wizara husika na Waziri Mkuu walikuwa wakihimiza Tanesco kukamilisha mchakato wa kumpata mzabuni haraka, jambo ambalo hakikuwakosha, maana ni jambo ambalo lilikuwa kwenye mujibu wao kuona nchi haiingii gizani kwa manufaa ya kiuchumi na ya kiusalama. Pia kwa umuhimu wa umeme kiuchumi na kiusalama suala la kupata mitambo ya kufua umeme wa dharura lililozungumzwa na kupata vikao vyote muhimu vya serikali ngazi ya Taifa likiwemo baraza la mawaziri.

Sinema zaidi ya kisiasa ilikuja kubainika katika mambo makubwa matatu. Kwanza ni kumtaka Waziri Mkuu apime na kuwajibika katika jambo ambalo halibainishi kosa lolote kwake, kiutawala wala kisiasa. Pili mabishano ya wanasiasa juu ya kutumia au kutoendelea kutumia mitambo ya DOWANS. Tatu mabishano ya wanasiasa juu ya kulipa au kutolipa kampuni ya DOWANS. Waliokuwa wanashikilia suala hili ni vyama vya upinzani hasa CHADEMA.

Ili kulinda heshima ya serikali nzima na chama tawala CCM, na pia ili kuepuka mgawanyiko miongoni mwa wanachama, wananchi na viongozi, Lowassa aliamua kujiuzulu nafasi ya Waziri Mkuu.

Kuhusu hoja ya kulipwa DOWANS na kuendelea kutumika kwa mitambo ambayo ililetwa na DOWANS, jambo hilo lilikwenda kwenye mabaraza ya kimataifa[onesha uthibitisho] na kuonekana wana haki ya kulipwa na mitambo iliyodaiwa na wanasiasa kuwa haifai ndiyo inayoendelea mpaka leo kufua umeme.

Uchaguzi mkuu 1995[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 1995 Edward Lowassa aliamua kuingia katika mchakato wa kumpata mgombea urais kwa tiketi ya CCM. Wakati huo Lowassa aliombwa na Umoja wa Vijana kupitia kikao cha baraza kuu la Taifa achukue fomu akiwa miongoni mwa wana CCM wanne ambao vijana waliamini wataweza kulisaidia Taifa kupiga hatua za haraka kuelekea maendeleo endelevu, wengine waliokuwa wametajwa na Umoja wa vijana ni Salim Ahmed Salim, Laurance Gama na jaji mstaafu Mark Bomani.

Katika hatua ya kuchagua majina 3 kati ya majina 11 yaliyoomba nafasi hiyo, Lowassa akawa hakupendekezwa, lakini hakununa wala kususa bali aliamini kuwa mwanamapinduzi mwenzie Jakaya Mrisho Kikwete ataweza kutekeleza dhamira aliyokuwa nayo ya kuwaletea Watanzania maendeleo, hivyo alirudi kwa makundi mbalimbali wakiwemo vijana wa CCM ambao walihoji kwa nini ameenguliwa, na yeye kwa utii mkubwa kwa CCM aliwataka vijana na viongozi wengine waheshimu maamuzi ya chama na kumuunga mkono Kikwete. Ikumbukwe kuwa mwana-CCM mwingine aliyekuwa anakubalika kwa umma Lowassa aliondoka mapema CCM kwa sababu ndogo tu ya kubadilishiwa wizara na kuamua kwenda chama cha NCCR mageuzi ambako aligombea uraisi kwa chama hicho na kuleta upinzani mkubwa.

Yapo maneno ya baadhi ya wanasiasa kwamba kutoteuliwa kugombea kwa Lowassa kulitokana na kuonekana anamiliki fedha nyingi akiwa na muda mfupi kwenye utumishi wa umma, lakini pia inasemekana kuwa wale waliohoji kukatwa kwa jina lake kwenye kikao cha Halmashauri kuu ya Taifa, majibu yalikuwa, CCM iliamua kupeleka majina matatu kwenye mkutano mkuu ili wachague moja katika uwakilishi huo wa majina: walipenda apatikane mtu mzima mmoja, mwenye umri wa kati mmoja na kijana mmoja, watu hao ni mzee David Msuya ambae ni mtu mzima, Benjamini Mkapa ambae umri wake ulikuwa wa kati na kijana ambae ni Jakaya Kikwete.

Lakini maneno hayo ya baadhi ya wanasiasa hayakuishia hapo: wakadai baada ya Rais Mkapa kuchaguliwa, hakumteua Lowassa kwa kuwa aliagizwa na Mwalimu Nyerere[onesha uthibitisho] asimteue mpaka achunguzwe kama uwezo kiasi wa fedha alionao unatokana na mapato halali, kama siyo halali asimteue. Mwaka 1997 Rais Mkapa akamteua Lowassa kuwa Waziri wa nchi, ofisi ya makamu wa Rais mazingira.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]