Majadiliano:Edward Ngoyai Lowassa
Kampeni imepamba moto, lakini je, iwe kazi ya Wikipedia pia? --Riccardo Riccioni (majadiliano) 12:19, 1 Agosti 2015 (UTC)
- Hahaha.. Kuna mtu katia ushabiki?--MwanaharakatiLonga 13:23, 1 Agosti 2015 (UTC)
- Labda kidogo... --Riccardo Riccioni (majadiliano) 14:09, 1 Agosti 2015 (UTC)
- Kumbe! Sina habari..--MwanaharakatiLonga 19:29, 1 Agosti 2015 (UTC)
Hatutaki kempeni hapa
[hariri chanzo]Mtumiaji mpya alifanya mabadiliko makubwa kwenye makala hii. sehemu nakubali maana waandishi wa mbele walimsifu kwa namna isiyolingana na kanuni za wikipedia:Msimamo wa kutopendelea upande; Kweche aliondoa sifa za aina hii lakini aliendelea kuongeza kashfa kama vile madai ailiiba. Ilhali inafamika kuna watu wanaodai yeye ni bora na wengine wanaomshtaki, hapa si mahali pa kurudia wala sifa wala kashfa. Inakubalika kutoa taarifa juu ya madai ya kila upande lakini hapo ni lazima kuweka pia vyanzo kwa madai (nani alidai nini, pamoja na mahali (gazeti, tovuti) ambako madai haya yalitangazwa. Mengine haikubaliki.
Ninafupisha sa makala na kuilinda. Kweche anapokea onyo. Kipala (majadiliano) 18:24, 12 Agosti 2015 (UTC)
- Nadhani umefupisha mno... Baadhi ya habari zilikuwa muhimu, ila ungekata sifa zisizokubaliwa na wote. Amani kwako!--Riccardo Riccioni (majadiliano) 07:22, 13 Agosti 2015 (UTC)
- Samahani kama nimezidi na kufuta kazi zako pia. Tufanyeje? Niliona mambo ya Kweche yasibaki, lakini kuacha sifa zilizokuwepo awali - basi nimesikia ni kama kuchukua msimamo upande mwingine. Ambacho sikutaka. Kwa hiyo - turudie? Kipala (majadiliano) 15:11, 13 Agosti 2015 (UTC)
- Sasa ninaanza kuelewa dukuduku la Mzee Kipala. Nimeisoma makala vizuri. Huyu bwana anamfanyia Kampeni Lowassa na amemsafisha vya kutosha. Haifai kabisa.. Bora makala irudishwe katika umbo lake la awali. Khaaa! Hapana!--MwanaharakatiLonga 08:24, 14 Agosti 2015 (UTC)
- Mimi ndimi niliyeanza kupunguza sifa za Lowassa katika ukurasa huo nikasema hatutaki kampeni. Ila naona sasa habari imebaki pungufu, kumbe hata sehemu juu ya Dowans inamsafisha. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 07:31, 15 Agosti 2015 (UTC)
Ulinzi
[hariri chanzo]Nimelinda makala sasa baada ya nyongeza ndefu na umo liliharibika kwa njia ya kuhariri kwa mobile edit. Sijachungulia yaliyomo yake. Kipala (majadiliano) 13:07, 20 Oktoba 2015 (UTC)
- Nimepanga makala upya kufuatana na mwendo wa miaka; sehemu kuhusu Richmond nimebadilisha kwa kuchukua tafsiri ya sehemu husika katika makala ya enwiki, ile iliyokuwepo kwangu haikueleweka vema . Kipala (majadiliano) 14:47, 20 Oktoba 2015 (UTC)