United People's Democratic Party
Mandhari
United People's Democratic Party (UPDP) ni chama cha siasa nchini Tanzania kilichosajiliwa rasmi tarehe 4 Februari 1993.
Katika Uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 chama hakikumsimamisha mgombea wa kiti cha urais na badala yake kilimuunga mkono mgombea wa chama cha National Convention for Construction and Reform-Mageuzi (NCCR-Mageuzi) kilichomsimamisha Sengondo Mvungi ambaye alipata asilimia 0.49% ya kura zote
Katika uchaguzi wa mwaka 2015 kilimsimamisha Fahmi Dovutwa kama mgombea wa urais.[1]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Dovutwa survives road accident". Daily News. 25 Oktoba 2015. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-06-16. Iliwekwa mnamo 2020-09-10.
{{cite news}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)