Nenda kwa yaliyomo

Mkoa wa Dodoma

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Dodoma
Mahali pa Mkoa wa Dodoma katika Tanzania
Mkoa wa Dodoma

Mkoa wa Dodoma ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye postikodi namba 41000[1]. Uko katikati ya nchi na umepakana na mikoa ya Manyara, Morogoro, Iringa na Singida.

Eneo lote la mkoa lina km² 41,310. Sehemu kubwa ni nyanda za juu kati ya mita 830 hadi 2000 juu ya UB.

Katika sensa ya mwaka 2022, idadi ya wakazi wa Mkoa wa Dodoma ilihesabiwa kuwa 3,085,625. [2]

Kuna wilaya nane zifuatazo: Bahi, Chamwino, Chemba, Dodoma Mjini, Kondoa, Kondoa Mjini, Kongwa, Mpwapwa. Wilaya ya awali ya Dodoma Vijijini imegawiwa katika wilaya mpya za Chamwino na Bahi. Mnamo Machi 2012 ilianzishwa wilaya mpya ya Chemba. Pia Wilaya ya Kondoa imegawiwa sehemu mbili.

Mawasiliano

[hariri | hariri chanzo]

Mawasiliano ni mazuri kwa barabara ya lami kuanzia mji wa Dodoma kwenda Morogoro - Daressalaam, barabara zingine ni za udongo to pamoja na njia kuu kuelekea Tanzania ya Magharibi - Rwanda - Kongo. Pia hali ya barabara ya kale ya "Cape - Cairo" inayovuka Dodoma kutoka kazkazini (Arusha - Kondoa ) kwenda kusini ni nzuri kwa kiwango cha lami. Kuna pia njia ya Reli ya Kati kutoka Daressalaam kwenda Kigoma yenye matatizo ya mara kwa mara. Dodoma mjini kuna uwanja wa kitaifa wa ndege.

Hali ya hewa na kilimo

[hariri | hariri chanzo]

Kwa jumla Dodoma haina mvua nyingi isipokuwa sehemu za wilaya za Mpwapwa na Kondoa. Hivyo hasa mazao yasiyotegemea sana mvua hulimwa kama vile mtama, wimbi, muhogo; kilimo cha mahindi hupatikana mara kwa mara na matatizo ya kukosa mvua. Mazao ya sokoni ni karanga alizeti na simsim. Dodoma ni pia mwanzo wa ustawishaji wa mizabibu na uzalishaji wa divai katika Tanzania.

Kutokana na hali ya hewa mifugo ni mingi (ng'ombe 1,600,000, mbuzi 954,000, kondoo 274,000, nguruwe 23,000, kuku takriban 1,400,000). Idadi ya mifugo imeongeza tatizo la mmomonyoko wa ardhi katika sehemu za mkoa.

Wakazi na utamaduni

[hariri | hariri chanzo]

Idadi kubwa ya wakazi asilia ni Wagogo.

Kongwa kuna Wakaguru, Wagogo, na Wamasai; na Mpwapwa kuna Wahehe, Wagogo, na Wakaguru.

Kondoa kuna Warangi na pia Wasandawe wanaotumia lugha ya aina ya Khoikhoi. Babu zao wamewahi kukaa eneo la Tanzania kabla ya kuingia kwa Wakushi, Wabantu na Waniloti. Kondoa kuna pia sehemu yenye michoro ya kale juu ya uso ya miamba ya aina ya Khoikhoi inayofanana na sanaa ya kale huko Zimbabwe au Afrika Kusini.

Majimbo ya bunge

[hariri | hariri chanzo]

Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. "Nakala iliyohifadhiwa" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2020-03-21. Iliwekwa mnamo 2017-09-23.
  2. https://www.nbs.go.tz


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Dodoma bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mkoa wa Dodoma kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.