Mkoa wa Simiyu
Jump to navigation
Jump to search
Mkoa wa Simiyu ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania,wenye postikodi namba 39000 [1]. Ulianzishwa rasmi Machi 2012 kwa kumega mkoa wa Shinyanga upande wa mashariki[2].
Makao makuu yako Bariadi.
Wakazi[hariri | hariri chanzo]
Kadiri ya sensa ya mwaka 2012, wakazi walikuwa 1,584,157,[3] kukiwa na ongezeko la 1.8% kwa mwaka katika miaka 2002-2012[3].
Msongamano wa watu ni 63 kwa kilometa mraba.[3]
Kabila kubwa ni lile la Wasukuma.
Wilaya[hariri | hariri chanzo]
Mkoa huo mpya una wilaya zifuatazo: Bariadi, Busega, Maswa, Meatu, Itilima.
Majimbo ya bunge[hariri | hariri chanzo]
Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:
- Bariadi : mbunge ni Andrew Chenge (CCM)
- Busega : mbunge ni Raphael Chegeni (CCM)
- Itilima : mbunge ni Njalu Silanga (CCM)
- Kisesa : mbunge ni Luhaga Mpina (CCM)
- Maswa Mashariki : mbunge ni Stanslaus Nyongo (CCM)
- Maswa Magharibi : mbunge ni Mashimba Ndaki (CCM)
- Meatu : mbunge ni Salum Khamis Salum (CCM)
Tazama pia[hariri | hariri chanzo]
Tanbihi[hariri | hariri chanzo]
- ↑ Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2018-08-05. Iliwekwa mnamo 2018-02-01.
- ↑ Staff. "Tanzania: State Gazettes New Regions, Districts", 9 March 2012.
- ↑ 3.0 3.1 3.2 Population Distribution by Administrative Units, United Republic of Tanzania, 2013. Jalada kutoka ya awali juu ya 2013-05-02. Iliwekwa mnamo 2017-08-22.
Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]
![]() | |
---|---|
Arusha | Dar es Salaam | Dodoma | Geita | Iringa | Kagera | Katavi | Kigoma | Kilimanjaro | Lindi | Manyara | Mara | Mbeya | Morogoro | Mtwara | Mwanza | Njombe | Pemba Kaskazini | Pemba Kusini | Pwani | Rukwa | Ruvuma | Shinyanga | Simiyu | Singida | Songwe | Tabora | Tanga | Unguja Kaskazini | Unguja Kusini | Unguja Mjini Magharibi |