Mkoa wa Iringa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Mji wa Iringa
Mahali pa Mkoa wa Iringa katika Tanzania
Wilaya za Mkoa wa Iringa na mikoa jirani

Mkoa wa Iringa ni moja kati ya mikoa 26 za Tanzania. Upo katikati ya nchi, kidogo upande wa kusini. Makao makuu yako katika manisipaa ya Iringa. Umepakana na mikoa ya jirani ya Morogoro, Ruvuma, Mbeya, Singida na Dodoma.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Mkoa wa Iringa uko katika Nyanda za Juu za Kusini mwa Tanzania. Mkoa huu unapakana na ukanda mkavu wa kati wa Tanzania katika upande wa kaskazini na kupakana kusini na Ziwa Nyasa. Mkoa wa Iringa umetanda kati ya latitudo 7º 05˝ na 12º 32˝ kusini, na longitude 33º 47˝ hadi 36º 32˝ mashariki mwa Meridian. Ziwa Nyasa linatenganisha Mkoa wa Iringa na nchi ya Malawi upande wa kusini Magharibi mwa Tanzania.

Hadi mwaka 2012 Mkoa wa Iringa ulikuwa na eneo lenye ukubwa wa jumla ya km² 58,936. Wastani wa asilimia 74 ya eneo hili linafaa kwa shughuli za kilimo ambalo ni sawa na km² 43,935. Eneo linalobakia la km2 15,001 ni eneo la maji, hifadhi ya mbuga za wanyama, milima na misitu.

Tangu mwaka 2012 maeneo ya Mkoa wa Njombe yalitengwa na Iringa na kuwa mkoa mpya kwa hiyo eneo la Iringa limepungua kilomita za mraba 21,347.

Wakazi[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 2012 palikuwa na wakazi 941,238 [1] katika wilaya zifuatazo: Iringa Kijijini (wakazi 254,032), Mufindi (wakazi 265,829), Kilolo (wakazi 218,130), Iringa Mjini (wakazi 151,345), na Mafinga Mjini (wakazi 51,902).

Makao makuu yako Iringa mjini.

Wenyeji wa mkoa ni hasa kati ya makabila yafuatayo: Wahehe, Wabena, Wakinga, Wapangwa na Wawanji.

Mwaka 2010 mkoa umemegwa na kuzaa mkoa wa Njombe upande wa kusini.

Majimbo ya bunge[hariri | hariri chanzo]

Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Sensa ya 2012, Iringa Region

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]


 
Mikoa ya Tanzania
Bandera Tanzania
Arusha | Dar es Salaam | Dodoma | Geita | Iringa | Kagera | Katavi | Kigoma | Kilimanjaro | Lindi | Manyara | Mara | Mbeya | Morogoro | Mtwara | Mwanza | Njombe | Pemba Kaskazini | Pemba Kusini | Pwani | Rukwa | Ruvuma | Shinyanga | Simiyu | Singida | Tabora | Tanga | Unguja Kaskazini | Unguja Kusini | Unguja Mjini Magharibi