Nenda kwa yaliyomo

Iringa (mji)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Manisipaa ya Iringa)


Iringa
Iringa is located in Tanzania
Iringa
Iringa

Mahali pa mji wa Iringa katika Tanzania

Majiranukta: 7°46′12″S 35°41′24″E / 7.77000°S 35.69000°E / -7.77000; 35.69000
Nchi Tanzania
Mkoa Iringa
Wilaya Iringa Mjini
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 202,490
Iringa, 1906

Iringa ni mji mkubwa mojawapo kusini mwa Tanzania wenye hadhi ya manisipaa. Ndiyo makao makuu ya Mkoa wa Iringa na eneo lake linaunda wilaya ya Iringa mjini.

Idadi ya wakazi ni 202,490 (sensa ya mwaka 2022 [1]).

Jina la Iringa lilimaanisha "mahali palipozungukwa na ukuta" kwa maana ya boma. Iringa ya kwanza ilikuwa Kalenga ya leo ambayo wakati wa vita ya Wajerumani dhidi ya Wahehe ilipanuliwa na kuimarishwa na Mtemi Mkwawa wa Wahehe kuanzia mwaka 1887 na kubomolewa na Wajerumani tarehe 31 Oktoba 1894. Mji mpya ulianzishwa na Wajerumani mwaka 1892 kama kituo cha kijeshi juu ya mlima unaotazama mto Ruaha bondeni.

Mji uko kando ya barabara kuu ya TANZAM; kuna usafiri wa kila siku kwenda Dar es Salaam na Mbeya. Njia kwenda Dodoma ni sehemu ya barabara ya kale ya "Cape-Cairo" kati ya Rasi ya Afrika Kusini na Kairo wa Misri na katika miaka ya 2010 imetiwa lami.

Kuna viwanda mbalimbali, hospitali, chuo kikuu na ofisi kuu za dayosisi za Kanisa Katoliki, Walutheri (KKKT) na Waanglikana.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Kata za Wilaya ya Iringa mjini - Tanzania

Gangilonga | Igumbilo | Ilala | Isakalilo | Kihesa | Kitanzini | Kitwiru | Kwakilosa | Makorongoni | Mivinjeni | Mkimbizi | Mkwawa | Mlandege | Mshindo | Mtwivila | Mwangata | Nduli | Ruaha


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Iringa bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Iringa (mji) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.