Cosato Chumi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Cosato David Chumi (amezaliwa 28 Julai 1974) ni mwanasiasa Mtanzania na mwanachama wa Chama cha kisiasa cha CCM. Amechaguliwa kuwa mbunge wa Mafinga Mjini kwa miaka 20152020. [1]

Alizaliwa katika Wilaya ya Mufindi. Alijiunga na elimu ya msingi mwaka 1984 na kuhitimu mwaka 1990 katika shule ya msingi Mkombwe. Baadae akachaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika katika shule ya sekondari Lugalo nakuhitimu mwaka 1994, baadae akachaguliwa kujiunga na kidato cha tano na sita katika shule ya sekondari ya Mkwawa high school na kuhitimu mwaka 1997.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Tovuti ya Bunge la Tanzania, iliangaliwa Mei 2017