Mkoa wa Mbeya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Mkoa wa Mbeya
Mahali pa Mkoa wa Mbeya katika Tanzania
Mahali pa Mkoa wa Mbeya katika Tanzania
Majiranukta: 2°45′S 32°45′E / 2.75°S 32.75°E / -2.75; 32.75
Nchi Tanzania
Wilaya 9
Mji mkuu Mbeya
Serikali
 - Mkuu wa Mkoa Albert.Chalamila
Eneo
 - Mkoa 63,617 km²
Idadi ya wakazi (2002)
 - 2,070,046
Tovuti: http://www.mbeya.go.tz/

Mkoa wa Mbeya ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye Postikodi namba 53000, ukipakana na Zambia na Malawi, halafu na mikoa ya Rukwa, Tabora, Singida na Iringa, mbali na mkoa mpya wa Songwe uliomegwa kutoka ule wa Mbeya upande wa magharibi mwaka 2016.

Kabla ya kugawiwa kulikuwa na wilaya 9 zifuatazo: Mbeya Mjini, Mbeya Vijijini, Rungwe, Kyela, Ileje, Mbozi, Chunya, Momba na Mbarali.

Tangu 2016 mkoa umekuwa na wilaya za Busekelo, Chunya, Kyela, Mbarali, Mbeya Mjini, Mbeya Vijijini na Rungwe.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Mbeya ni kati ya maeneo yanayopendeza kabisa ndani ya Tanzania ikiwa na sehemu za Ziwa la Nyasa, Ziwa Rukwa, Mlima ya Mbeya, Mlima ya Rungwe, Uwanda wa juu wa Uporoto, Uwanda wa Usangu ingawa haukufikiwa bado na utalii.

Wilaya ya Rungwe ni eneo lenye mvua nyingi katika Tanzania. Mkoa wa ujumla ni mojawapo kati ya mikoa yenye kilimo kizuri inayotoa mazao ya kulisha taifa. Lakini maeneo makubwa ya Wilaya ya Chunya ni makavu.

Wilaya ya Chunya ina madini mbalimbali hasa dhahabu. Wenyeji wa wilaya ya Chunya ni Wabungu na waishio huko zaidi ni Wanyiha.

Mbeya na Mbozi kahawa hupandwa. Rungwe pana chai nyingi, pamoja na Rungwe na Chimala hulimwa mpunga. Nyanda za juu kuna nafaka na viazi.

Kijiolojia mkoa wa Mbeya ni eneo la kukutana kwa mikono miwili ya Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki inayoendelaea hapa katika ziwa Nyasa.

Maziwa na mito[hariri | hariri chanzo]

Mkoa wa Mbeya inapakana na maziwa mawili makubwa ndiyo Ziwa Nyasa na Ziwa Rukwa. Hasa milima yenye asili ya volkeno ya wilaya ya Rungwe inyajaa maziwa ya kasoko.

Mito mikubwa ni Songwe na Kiwira. Chanzo cha mto Ruvuma kiko pia Mbeya katika tambarare ya Usangu.

Majimbo ya bunge[hariri | hariri chanzo]

Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:

Waandishi toka mkoa wa Mbeya[hariri | hariri chanzo]

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]